UCHAGUZI KAMATI YA UONGOZI TPLB
Uchaguzi
wa Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania Bara utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam.
Fomu
kwa ajili ya wagombea zitaanza kutolewa Agosti 17, 2017 kwenye ofisi za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mwisho wa kuchukua na
kurudisha fomu kwa wagombea ni saa 10.00 jioni Agosti 23, mwaka huu.
Nafasi
zitakazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watatu
kuwakilisha klabu za Ligi (PL), Wajumbe wawili wa kuwakilisha klabu za
Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Mjumbe mmoja wa kuwakilisha klabu za
Ligi Daraja la Pili (SDL).
Ada
ya fomu kwa nafasi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ni Sh 200,000
(Shilingi lakini mbili) wakati nafasi nyingine zilizobaki ni Sh 100,000
(Shilingi laki moja).
Uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu husika.
Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au Marais wa klabu husika.
Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.
MALALAMIKO YA KLABU KATIKA USAJILI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea malalamiko kutoka baadhi ya
timu na vituo vya kuibua na kukuza vipaji vya soka zikidai fidia baada
ya wachezaji wao kusajiliwa na klabu nyingine msimu wa 2017/18.
Jana
Agosti 14, 2017 ilikuwa siku ya mwisho kwa timu na vituo vya kuibua na
kukuza vipaji kuwasilisha malalamiko yao TFF kuhusu fidia za mafunzo;
ada ya usajili; ada za maendeleo na kuvunjwa kwa mikataba kutoka katika
timu walizochezea hadi msimu uliopita.
TFF
imepokea malalamiko ya Kagera Sugar ya Kagera dhidi ya Azam FC ya Dar
es Salaam kuhusu mchezaji Mbaraka Yussuf wakati Majimaji ya Songea pia
imelalamika Azam kuhusu mchezaji Idd Kipangwile.
Alliance
ya Mwanza imelalamikia Pamba pia ya Mwanza kuhusu mchezaji Juma Nyangi
ambako madai hayo yamekwenda mbali zaidi yakisema kuwa mchezaji husika
amebadili jina kwa lengo la kudanganya.
Kwa
upande wake, African Lyon imeondokewa na wachezaji 19 na inadai fidia
katika timu, wachezaji kwenye mabano za Majimaji (Saleh Malande); Lipuli
(Hamad Manzi, Lambele Reuben na Mussa Nampoka); Young Africans (Rostand
Youthe Jehu); Tusker FC (Abdul Hilal) na Ndanda kwa wachezaji Hamad
Tajiri na Baraka Majogoo.
Madai
mengine ni dhidi ya Coastal Union kwa wachezaji Baraka Jaffary, Omary
Salum, Raizen Hafidh na Fred Lewis huku madai mengine ni kwa Kagera
Sugar kwa wachezaji Omar Abdallah, Abdallah Mguhi na Vicent Ludovic na
Alhaji Zege .
Madai
mengine ni dhidi ya timu ya Kinondoni Municipality Council (KMC) ambayo
imewasajili Halfan Twenye, Yussuf Abdul na Rehani Kibingu wakati
Singida United inalalamikiwa kumsajili Miraji Adam ilihali Njombe Mji
inadaiwa fidia kwa kumsajili mchezaji Salum Juma.
Malalamiko
mengine ni ya Kisa Academy ya Kinondoni, Dar es Salaam dhidi ya timu za
Mbeya City (Idd Seleman); Majimaji (Jafar Mohammed); Mbao (Ally
Rashid); Stand United (Said Mbati) na Friends Rangers (Hassan Abubakar).
Madai
mengine dhidi ya timu za Coastal Union (Abubakar Nyakarungi na Ahmed
George); The Mighty Elephant (Maliki Hamad); Kagera Sugar (Hussein Idd)
na Azam FC (Omary Maunda).
Kikao
cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kinatarajiwa kuketi
Jumapili kupitisha usajili lakini kabla kitapitia malalamiko hayo na
kuchukua uamuzi.
MAANDALIZI MECHI YA NGAO YA HISANI
Maandalizi
ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaowakutanisha Mabingwa wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara 2016/17, Young Africans na Mabingwa wa Kombe la
Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup), Simba yanakwenda vema.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwatangazia umma kuwa
viingilio katika mchezo huo vimepangwa katika makundi manne.
Sehemu
ya VIP ‘A’ tiketi zake ni Sh 25,000; sehemu ya VIP ‘B’ na ‘C’ Sh
20,000; Viti vya Rangi la Chungwa Sh 10,000 na mzunguko kwa vitu vya
rangi za bluu na kijani ni Sh 7,000.
Tiketi
zimeanza kuuzwa leo Jumanne Agosti 15, 2017 ili kuwapa fursa wadau wa
mpira wa miguu kununua tiketi mapema kujipeusha na usumbufu.
KIKAO KLABU ZA LIGI DARAJA KWANZA
Viongozi
wa Klabu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL), wanatarajiwa kuwa
na kikao na uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB), kitakachofanyika Ijumaa
Agosti 8, 2017 kuanzia saa 3.00 asubuhi kwenye Hosteli za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Pamoja
na mambo mengine, kikao hicho kitakuwa maalumu kwa ajili ya kujadili
Ligi Daraja la Kwanza lakini pia kutoa semina kwa viongozi hao kuhusu
Leseni za Klabu (Club License).
TFF
inatoa wito kwa viongozi wa juu wa klabu kuhudhuria kikao hicho muhimu .
TFF ingependa kusisitiza kuzingatia muda wa kuanza kikao.
EmoticonEmoticon