UVCCM YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTENGANISHA SIASA NA MAENDELEO

August 16, 2017
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akionyesha ilani ilani ya CCM mwaka 2015-2020 na maelekezo ya namna ya utekelezaji wakati akizungumza na Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Ndg Abdallah Rashid Ali akielezea namna Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inavyotekeleza ilani ya CCM mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Na Mathias Canal, Kusini Pemba

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa kauli moja Umewataka watumishi wa Umma kote nchini Kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 kwa kutenganisha Siasa na shughuli za maendeleo. 

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 15, 2017 na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) alipokuwa akizungumza na Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Shaka ametilia mkazo zaidi kwa kuwataka Watumishi wa Serikali kutenganisha siasa na Majukumu ya kazi kwa Wananchi ili kuwaletea maendeleo pasina kuwabagua kwa dini, kabila ama utofauti wa itikadi za vyama vya kisiasa.

Alisema kuwa litakuwa Jambo la aibu tena lisilovumilika kwa Viongozi wa Umma kushughulika na Mambo ya siasa kwani hizo Ni kazi za vyama vya siasa ambavyo hata vyama vya siasa vina mipaka katika kufanya siasa.

Shaka Alisema kuwa watumishi wa Umma wamepewa dhamana kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli hivyo Ni matarajio ya Chama Cha Mapinduzi CCM na Serikali, watumishi wote Kusimamia na kuwajibika ili Kutekeleza imara ilani kwa utayari.

Alisema kuwa ilani ya CCM imeielekeza Serikali kufanya Mambo mengi ya Maendeleo ambayo kwa asilimia kubwa tayari yameanza kutekelezwa kwa usimamizi mzuri wa Rais Magufuli.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo chini ya CCM hivyo kila kiongozi aliyeajiriwa na Serikali Ana jukumu moja kubwa la Kutekeleza ilani kwa umakini mkubwa kwa maslahi mapana ya Taifa.

"Kama kuna mtumishi asiyefanya hivyo basi ni wazi kuwa hastahili kuendelea kuwa kwenye nafasi yake"

"Tunakuwa na mipango mingi lakini utekelezaji wake unasuasua kwa kisingizio Cha bajeti ndugu zangu ifike Wakati tuwe na bajeti inayotekelezwa na itekelezwe kwa umakini, uangalifu na weledi Mkubwa" Alisema Shaka

Alisema kuwa watumishi wa serikalini wanapaswa kubainisha vyema Mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa manufaa ya Wananchi pasina kuwabagua zaidi ni kukubali kuwa wawajibikaji wazuri.

Katika Hatua nyingine UVCCM Taifa imempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohed Shein kwa maendeleo endelevu aliyoyafanya katika kipindi Chake tangu amekuwa Rais wa Zanzibar kwa kuimarisha Huduma za uwanja wa Ndege, uchumi wa Pemba umeimarika, fursa za uwekezaji sio Kama kipindi kilichopita.

Umoja huo umesisitiza kuwa Ni vyema wasaidizi wa Rais kumsaidia kwa vitendo sio maneno kwani Ni Lazima Viongozi kuwa na uthubutu na uwajibikaji.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »