Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa mshtuko na masikitiko
makubwa msiba wa Linah George Mwakyembe - mke wa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Linah amefariki usiku wa kuamkia jana Julai 15, mwaka huu kwenye
Hospitali ya Aga Khan alikokuwa akipatiwa matibabu. Mipango ya mazishi
inafanyika nyumbani kwa Waziri Mwakyembe, Kunduchi jijini Dar es Salaam.
“Hakika
nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Linah ambaye nimejulishwa kimetokea
jana katika Hospitali. Kifo hiki kimeleta huzuni kubwa kwa wanafamilia
ya michezo hususani mpira wa miguu.
“Natuma
salamu za rambirambi kwako Mheshimiwa Waziri wetu mpendwa. Hakika
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huu. Ni pigo kubwa
katika familia, lakini kwa wakati huu mgumu, Mheshimiwa Mwakyembe,
familia yake, ndugu jamaa na marafiki hawana budi kuwa watulivu na wenye
subira,” amesema Karia.
“Naungana
na familia ya Mwakyembe katika msiba huu ambao pia ni msiba wetu sote
wanafamilia ya mpira wa miguu. Naungana nao pia kumwomba Mwenyezi Mungu
aiweke peponi roho ya Marehemu Linah Mwakyembe. Amina.”
EmoticonEmoticon