Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu
Jenista Mhagama kushoto akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu
(katikati) na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng Issa kulia
wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu
Jenista Mhagama kushoto akikata utepe(ribbon) kuashiria kuzindua wa
taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi
ya Julai 2015 mpaka April 2017 wakati wa Kongamano la Pili la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,(katikati) Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu na kulia
ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu
Jenista Mhagama kushoto akionyesha kitabu cha taarifa ya utekelezaji wa
sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April
2017 mara baada ya kuzindua taarifa hiyo wakati wa Kongamano la Pili la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,(katikati) Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu na kulia
ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu
Jenista Mhagama kushoto akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Joel
Bendera taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi
kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 mara baada ya kuzindua taarifa
hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng Issa.
Watanzania
wametakiwa kubadili fikra za kimtanzamo na kila mtu kutimiza wajibu
wake kwa lengo la kuunga mkono dhamira ya serikali ya awamu ya tano ili
kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha ustawi wa jamii.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu
Jenista Mhagama alisema hayo wakati alipokuwa akifungua Kongamano la
Pili la Uwezeshaji Watanzania Kiuchumi, kuwa watanzania wanatakiwa
kubadili fikra za kimtanzamo ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda, na
kuboresha ustawi wa jamii.
“
Nchi yetu imeamua kubadilisha mwelekeo wa uchumi wa nchi yetu na sisi
tunawajibu wa kubadili fikra za kimtanzano ili kufikia uchumi wa
viwanda,” aliongeza kusema Bi. Mhagama, ambaye alifungua kongamano hilo
kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Pia
aliwataka washiriki wa kongamano kwenda kushirikiana na wananchi katika
kuhakikisha suala la uchumi wa wananchi unakuzwa. Na aliwasisitiza
watumishi wa umma kuwa mfano katika kuchochea dhamira hiyo kwa kufanya
kazi kwa vitendo.
Alisema
serikali imeweka mikakati kabambe ya kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi
inayoendana na soko la ajira kupitia program mbalimbali ikiwemo ya
kuwafundisha vijana ujuzi waweze kutumika katika nguvu kazi. Na
aliwataka wakuu wa mikoa yote kuainisha fursa za kiuchumi na kumpatia
waziri mkuu ili zifanyiwe kazi.
Halikadhalika
aliitaka mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kuhakikisha fedha
zilizopo katika mifuko yao inawafikia watanzania waweze kukopa na
kuwekeza katika shughuli za uzalishaji na biashara. Kauli Mbiu ya
Kongamano hilo ni Wezesha Watanzania Kushiriki Uchumi wa viwanda.
Waziri
huyo pia alizidua taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji
wananchi kiuchumi ya julai 2015 mpaka April 2017. Pia alitoa vyeti na
vikombe kwa sekta umma na binafsi waliofanya vizuri katika kutekeleza
uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
(NEEC),Bi. Beng’I Issa alisema kongamano hilo lilikuwa la mafanikio kwa
kuwa lilishirkisha wadau wote na kwa sasa wanalenga kwenda kutekeleza
kwa vitendo majukumu yao.
“Kongamano
hili tumepatiwa agizo la kila Wilaya kuwa na kiwanda kimoja na sisi
tumejipanga kusimamia kwa vitendo,” na kuongea kusema viwanda huwezesha
mali ghafi kuongezwa thamani na kutoa ajira.
Sambamba
na hilo huongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo na kuwa chachu ya
uchumi wa nchi kwa kuwa kilimo kina nafasi ya kuajiri watu wengi zaidi
na kuongeza vipato vya wananchi.
Pia
kila halmashauri imepwa jukumu la kuainisha maeneo ya kufanyia biashara
zikiwa na miundombinu yote na kumpatia waziri mkuu hadi ifikapo Agosti
2017 ili yaweze kufanyiwa kazi.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na
Teknolojia (MJKNUAT), Profesa Dominic Kambarage alisema baraza linafanya
kazi kubwa na nzuri na inatekeleza sera ya uwezeshaji wananchi
kiuchumi.
”Kutokana
na kazi hii nzuri tuongeze nguvu ngazi ya mikoa na wilaya za kufanya
kazi kwa vitendo na maeneo ya biashara yatengwe wananchi wawe na fursa
za maeneo ya kufanyia biashara,”. Na taasisi za elimu ya juu na kati
ziboreshe mitaala yao kwa ajili ya vijana kuondoa tatizo la ajira.
EmoticonEmoticon