POLISI TANGA YAWAKAMATA WATANO KWA WIZI WA ZAIDI YA MILIONi 20 KWA NJIA YA MTANDAO

December 19, 2024


Na Paskal Mbunga, Tanga.

Jeshi la Polisi mkoani Tanga limefanikiwa kuwakamata watu watano kwa makosa ya wizi  wa zaidi ya sh milioni 20,390,000 kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Muchunguzi alisema watuhumiwa hao wamekatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali nchini.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Said Amiri aka mofisamchayungu (21),Amiri Athumani (24),Brayan Matina Mayunga (26) ambao wote ni wakazi wa Jijinj Dar Es Salaam.

Alisema pia Polisi imefanikiwa kukamata Wakala WA mitandao hiyo James John (24)  mkazi Dar na Peter Babuya (20) mkazi wa Arusha na ni mwanafunzi wa chuo cha Uhasibu Arusha.

Kamanda Muchunguzi alibainisha kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa Kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Jijini Dar na Masasi Mkoani Mtwara baada ya watuhumiwa hao kujifanya mawakala wa kijitegemea (Freelancers) wa kampuni za simu za Tigo,Voda na Airtel na kuiba kiasi hicho cha fedha Kwa njia ya mtandao mali ya Abdul Hemed Shedafa ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Kamanda huyo alisema kwamba baada ya kufanyika uchunguzi wa kitaalamu imebainika watuhumiwa walitumia mbinu za ulaghai ikiwemo kutumia namba za simu zilizosajiliwa Kwa majina mengine ili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo alisema Desemba 10 mwaka huu katika msako uliofanyika Kijiji cha Makuyuni Kata ya Makuyuni Tarafa ya Mombo walikamatwa watuhumiwa Wawili ambao ni Hashim Mohammed (46) dereva na mkazi wa Buguruni Malapa Dar na mwenzie Ramadhani Mbaruku (28) kondakta mkazi wa Tegeta (Dar) wakiwa wanasafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi Kwa kutumia gari yenye namba za usajili T.689 EJJ aina ya Coaster wakitokea Kilimanjaro kuelekea Jijini Dar Es Salaam.


Katika upekuzi wa gari Hilo watuhumiwa walikutwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi bunda 962 sawa na kilo 411.5 dawa hizo zikisafirishwa kwa lengo la kuingizwa sokoni.

Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.


Mwisho




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »