MKUTANO WA WAKUU WA MAGEREZA /TAASISI ZA UREKEBISHAJI ZA NCHI ZA SADC WAFANYIKA JIJINI DAR

June 11, 2017
wak1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni(wa pili toka kulia) akiwaongoza kuimba wimbo wa Taifa la Tanzania Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee(hawapo pichani). Wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, (wa kwanza kutoka kushoto) ni Mjumbe wa Sekretarieti ya SADC, Bw. Maemo Machete. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
wak2
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni kufungua rasmi mkutano huo wa siku moja.
wak3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee uliofanyika leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
wak4
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano huo toka nchi za SADC wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga.
wak5
Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao hicho kama inavyoonekana katika picha.
wak7
Wajumbe wa Mkutano huo toka nchi za SADC wakifuatilia majadiliano kama wanavyoonekana katika picha(katikati) ni Mkuu wa Magereza nchini Botswana, Silas Motlalekgosi.
wak8
. Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo akiteta jambo na Mjumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC, Bw. Maemo Machete.
wak9
Wajumbe wa kutoka Jeshi la Magereza Tanzania wakipitia baadhi ya nyaraka mbalimbali za Mkutano huo(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani, SACP. Boyd Mwambigu(katikati) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP. Mzee Ramadhan Nyamka(kushoto) ni SACP. Justine Kaziulaya.
wak11
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Magereza toka nchi za SADC. Wa tatu toka kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza).
wak10
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Magereza toka nchi za SADC. Wa tatu toka kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »