Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk.Harisson Mwakyembe wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa sh.bilioni 2.1 uliotolewa na Kampuni ya Bia ya SBL Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuidhamini timu ya Taifa Stars kwa miaka mitatu.
Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo na wanahabari.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk.Harisson Mwakyembe (katikati), akisisitiza kuhusu wadau kujitokeza kuchangia sekta ya michezo.
Makubaliano hayo yakisainiwa. Kulia ni Mwanasheria wa TFF, Emmanuel Muga na kushoto ni Mwanasheria wa SBL, Lusia Uinde.
Mkataba ukioneshwa baada ya kusainiwa.
Ni furaha baada ya kusainiwa kwa mkataba huo. Hapo unaoneshwa mbele ya wanahabari.
Mfano wa hundi yenye thamani ya sh.bilioni 2.1 ikioneshwa kwa wanahabari baada ya SBL kuikabidhi kwa TFF. |
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNIya Bia Serengeti (SBL) imeingia mkataba wa mitatu na Shirikisho la Mipira wa Miguu Tanzania (TFF) wathamani ya shilingi bilioni 2.1 ambao unaifanya kuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa-Taifa Stars.
Hii ni mara ya pili kwa SBL kuiunga mkono timu ya taifa baada ya kampuni hiyo kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu ilipoidhamini timu hiyo kati ya mwaka 2008 hadi 2011.
Katika makubaliano hayo ambayo yalisainiwa jijini Dar es Salaam jana na pande hizo mbili na Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie na Rais wa TFF Jamal Malinzi, kampuni ya SBL itapata fursa ya kutangaza biashara yake wakati wa mechi zote za Taifa Stars za nyumbani na ugenini.
Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo Weesie alisema uamuzi wa kampuni hiyo wa kuidhamini timu ya taifa unatokana na sera ya SBL ya kusaidia kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za ijamii ikiwemo michezo.
Alisema wanaunga mkono sekta ya michezo nchini na kubainisha kwamba michezo sio tu inaburudisha bali pia inaunganisha mashabiki na pia ni chanzo cha kipato kwa vijana.
“SBL inaona fahari kuidhamini timu yetu ya taifa kwa mara nyingine tumechukua hatua hii kwa kuwa tunaelewa mchango wa sekta ya michezo katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii " alisema.
Aidha Weesie aliongeza kuwa wanaamini kuwa udhamini wao huo utachangia kukuza vipaji vya vijana wetu pamoja na kuleta hamasa kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya taifa.
Rais wa TFF Jamal Malinzi aliishukuru SBL kwa kukubali kuidhamini Taifa Stars jambo ambalo alisema litasaidia katika kufanikisha maandalizi mazuri na ushiriki kikamilifu wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali, ndani na nje ya nchi.
“Udhamini wa SBL umekuja kwa wakati mwafaka, wakati ambapo timu yetu ya taifa ipo katika hatua za maandalizi kwa mashindano ya kikanda na kimataifa,” alisema Malinzi.
Hafla ya kusainiwa kwa udhamini huo ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk.Harisson Mwakyembe ambaye alitoa wito kwa kampuni zingine na watu binafsi wenye mapenzi na michezo kujitokeza na kutoa michango ya hali na mali ili kuendeleza sekta hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
EmoticonEmoticon