Washiriki Wa Tigo Reach For Change
Waliofanikiwa Kuingia Katika Mchujo Wa Mwisho Wakiwasilisha Wazo Lao Ubunifu
Mbele Ya Majaji Mapema Wiki Hii Katika Ofisi Za Makao Makuu Ya Tigo ,Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.
Majaji wa Tigo Reach for Change wakimsikliza kwa makini mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuingia katika mchujo |
Na Mwandishi Wetu
Mashindano ya mwaka huu ya Waleta mabadiliko ya kidijitali wa Tigo yamefikia katika hatua ya juu ya kuchagua washindani watano kufuatia mchakato wa mapitio ambao ulijumuisha waombaji 358. Shindano hili hufanyika kila mwaka na liko wazi kwa waombaji kutoka nchi nzima limejielekeza katika kuibua vijana mahiri walio na ubunifu wa miradi ya kidijitali inayoboresha maisha ya watu, hususani watoto kwa kutumia programu za kidijitali.
Vijana watano wanaoingia katika hatua ya fainali hupata nafasi ya kuhudhuria warsha ya maendeleo ya maudhui ya siku mbili pamoja na kuwasilisha miradi yao wakisubiri uthibitisho wa mwisho kutoka kwa jopo la wataalamu wa ndani na nje katika ujasiriamali na stadi za kidijitali.
Waleta mabadiliko wa Kidijitali wa Tigo ni wazo la Kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya Reach-for- Change ikiwa ni programu ya ushauri na kuunga mkono ambayo inawapa washindi fursa ya kuanzisha ujasiriamali endelevu katika maeneo ya elimu, ujumuishwaji wa kidijitali na shughuli za ujasiriamali.
Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo, Halima Okash alisema kuwa washindi wawili wa kwanza watapata fedha taslimu dola 20,000 (takribani shilingi milioni 44,000,000) kuwezesha utekelezaji wa maudhui yao.
“Miradi hii ina matokeo makubwa kijamii, inatoa masuluhisho halisi kwa matatizo yanayoikabili jamii na yana umuhimu katika kuboresha moja kwa moja maisha na hususani maisha ya watoto,” alisema Okash, akibainisha kuwa kampuni hiyo ya simu tayari imeshawasaidia wajasirimali kijamii tisa kupitia mkakati wa waleta mabadiliko wa Tigo (Tigo Digital Changemakers).
Huu ni mwaka wa sita ambapo Tigo na Reach-for-Change wanaendesha shindano la kutafuta wajasiriamali kijamii.
Mshindi wa mwaka huu atatangazwa Machi 9.
EmoticonEmoticon