Mkaguzi
wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe
(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango namna zoezi zima la uhakiki wa wastaafu kanda ya kaskazini
linavyokwenda kabla ya uzinduzi wa zoezi hilo. Zoezi hili ni kwa mikoa
ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
Zoezi
la kuhakiki wastaafu likiendelea katika Ofisi za Makao Makuu,
Halmashauri ya jiji la Arusha, Pichani ni baadhi ya wastaafu wakifanyiwa
uhakiki.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akifurahia
jambo na baadhi ya wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Hazina,
waliojitokeza kuhakikiwa wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika Ofisi
za halmashauri ya Jiji la Arusha, zoezi litakalo dumu kwa siku tano hadi
Ijumaa wiki hii katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Tanga,
Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akiongea
na baadhi ya wastaafu waliofika katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la
Arusha kwa ajili ya uhakiki ambapo wastaafu hao wameiomba serikali
iwaongezee kiwango cha pensheni wanacholipwa ili waweze kukabiliana na
hali ngumu ya maisha.
Baadhi
ya Wastaafu wanaolipwa Pensheni yao na Hazina, waliofika katika Ofisi
za Makao Makuu, Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya kuhakikiwa.
Baadhi
ya Wastaafu wanaolipwa Pensheni yao na Hazina, Livingstone Kisanga
(kulia) na Allen Kijazi, wakazi wa Arusha, wakisubiri kuhakikiwa katika
Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha, wakati wa zoezi la uhakiki wa
wastaafu hao linalofanyika katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini (Tanga,
Kilimanjaro, Arusha na Manyara).
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akihojiwa
na baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya
kuongea na wastaafu waliofika kwa ajili ya uhakiki, ambopo wastaafu
wengi wameridhishwa na zoezi hili la wanashukuru zoezi hili linaenda kwa
haraka kwani wengi wao wana nyaraka zote muhimu zinazohitajika.
Wawezeshaji
wa zoezi la uhakiki wakibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika. Kushoto kwake ni Mkaguzi wa
Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe na Mkaguzi wa Ndani
Mkuu Bw. Paison Mwamnyasi.
Mkaguzi
wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Mohamed Mtonga, akitoa ufafanunuzi kwa
wanahabari wa mkoa wa Arusha kuhusu masuala mbalimbali ya uhakiki wa
wastaafu wanaolipwa na Hazina, unaoendelea katika kanda ya Kaskazini,
mikoa ya Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro.
Mstaafu,
Mwanakombo Yusuph, mkazi wa eneo la Kaloleni, Jijini Arusha, akihojiwa
na Wanahabari mara baada ya kuhakikiwa katika ukumbi wa Halmashauri ya
Jiji la Arusha ambapo ameipongeza Serikali kwa kuendesha uhakiki huo
utakaosaidia kuhuisha daftari la wastaafu na kwa uamuzi wake wa kuwalipa
wastaafu kila mwezi badala ya miezi mitatu mitatu.
Bi.
Amina Msigiti (kulia) ambaye ni mstaafu anayelipwa na Wizara ya Fedha
na Mipango, akijiandaa kutia saini fomu yake ya uhakiki mbele ya Afisa
wa Hazina, Winfrida Moshi, kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la
Arusha.
EmoticonEmoticon