UTANGULIZI
Kuna
baadhi ya watu wanadai kuwa, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya
kuingilia maamuzi ya chama cha siasa, hivyo msimamo wake juu ya mgogoro
wa uongozi wa chama cha CUF ni batili. Napenda kutumia fursa hii
kuwafahamisha kuwa, Msajili wa hana mamlaka ya kuingilia uamuzi halali
uliofanywa na kikao halali cha chama cha siasa, Lakini, kama uamuzi ni
batili na kikao ni batili au uamuzi ni halali umefanywa na kikao batili
au uamuzi batili umefanywa na kikao halali, msajili hawezi kuutambua,
kwani Sheria ya Vyama vya Siasa inampa Msajili wa Vyama vya Siasa wajibu
wa kusimamia utekelezaji wa baadhi ya maamuzi ya chama cha siasa
ikiwamo suala la upatikanaji wa viongozi wa kitaifa wa chama cha siasa
kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama husika. Ni vyeme ieleweke wazi
kuwa kwa mujibu wa kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Usajili wa Vyama vya
Siasa uamuzi wa kufanya mabadiliko yoyote kwa viongozi wa kitaifa wa
chama cha siasa ni lazima upelekwe kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ili
atambue mabadiliko hayo.
Hivyo,
kuhusu mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF uliojitokeza kufuatatia
kujiudhuru kwa Profesa Lipumba ni kwamba, malalamiko na hoja
zilizowasilishwa kwa Msajiili wa Vyama vya Siasa na baadhi ya viongozi
wa CUF ikiwamo Profesa Lipumba zilikuwa za aina tatu, ambazo ni
zifuatazo:-
1. Kupinga utaratibu uliotumika kuendesha Mkutano Mkuu wa Taifa wa tarehe 21 Agosti, 2016;
2. Kujiuzulu na kutengua kujiuzulu uenyekiti wa taifa wa CUF; na
3. Kupinga uhalali wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi cha tarehe 28 Agosti, 2016 kilichofanyika Zanzibar na maamuzi yake.
Malalamiko
na hoja zote tajwa hapo juu zinahusu hatma ya baadhi ya viongozi wa
kitaifa wa chama cha CUF. Viongozi hao ni wafuatao:-
1. Profesa Lipumba ambaye aliandika barua ya kujiuzulu uenyekiti wa Taifa na kuitengua;
2. Mheshimiwa
Mgdalenda Sakaya Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara aliyesimamishwa
uanachama na Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa cha tarehe 28 Agosti,
2016;
3. Bwana
Abdul Kambaya, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Taifa ambaye pia
amesimamishwa uanachama na Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa cha
tarehe 28 Agosti, 2016; na
4. Bwana
Shashu Lugeye Katibu wa Baraza la Wazee ambaye alifukuzwa uanachama na
Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa cha tarehe 28 Agosti, 2016;
MSIMAMO WA SHERIA
Hivyo,
kwa kuwa kifungu cha 10(f) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258
kinahitaji chama cha siasa kuwasilisha orodha ya viongozi wake wa
kitaifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kifungu 8A(1) kinampa mamlaka
Msajili wa Vyama vya Siasa kuhifadhi taarifa za viongozi wa kitaifa wa
Vyama vya Siasa na Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Usajili wa Vyama vya
Siasa toleo namba 111 la mwaka 1992, inakitaka kila chama cha siasa
kuwasilisha taarifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa panapotokea
mabadiliko katika uongozi wa taifa. Hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa
anao wajibu wa kuhakikisha taarifa za mabadiliko ya uongozi anazoletewa
na chama cha siasa, ni sahihi kwa maana ya kuwa, yamefanywa na mamlaka
halali ya chama kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika, ili
kuepuka kupokea orodha ya mabadiliko ya uongozi wa kitaifa wa chama
ambayo si halali kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama.
Vifungu hivyo vinasema ifuatavyo:-
“10(f)
it has submitted the names of the national leadership of the party and
such leadership draws its members from both Tanzania Zanzibar and
Mainland Tanzania; …”
“8A.-(1)
There shall be a register of political parties into which names,
addresses and other particulars of registered political parties or
national leaders of political Parties shall be entered”
Kanuni ya 5(1) inasema ifuatavyo:-
“5-(1)
Where an office –bearer of a registered party ceases to hold office or a
person is appointed to be an office-bearer of a registered party, the
party shall, within fourteen days, send notice thereof to the
Registrar.”
Kwa
kuzingatia ulazima wa Msajili wa Vyama vya Siasa kujiridhisha kuwa,
mabadiliko yoyote katika uongozi wa kitaifa wa chama cha siasa
yamefanywa kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika, ndipo akubali
kufanya mabadiliko katika orodha ya viongozi wa kitaifa iliyopo katika
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, ndiyo maana ikawepo kanuni ya 13(1)
na 16 zinazompa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuhitaji maelezo
kutoka kwa chama cha siasa, kuhusu viongozi wa kitaifa wa chama cha
siasa. Kanuni hizo zinasema ifuatavyo, nanukuu:-
“13-(1) The Registrar may at any time require a party to submit to him a
return or report relating to the constitution, objects, office-bearers
or membership as well as the finances of the party.
2)
Every office-bearer and every person managing or assisting in the
management of a party shall forthwith comply with any requirement made
by the Registrar under paragraph (1) of this Regulation.”
“16.
In the event of a breach by a party of the provisions of Regulation
6,7,8,11,12 or 13, every office-bearer of the party concerned shall be
guilty of an offence and shall be liable on conviction to a fine not
exceeding thirty thousand shillings or to imprisonment for a term not
exceeding six months or to both such fine and imprisonment.”
Kwa
maana hiyo basi, Msajili wa Vyama vya Siasa anayo mamlaka ya
kushughulikia malalamiko na hoja tatu zilizowasilishwa kwake na baadhi
ya wanachama na viongozi wa CUF, kwa sababu malalamiko na hoja zote
zinagusa mabadiliko katika uongozi wa kitafa wa CUF.
Inaeleweka
kuwa, suala la uanachama wa chama cha siasa ni uhusiano wa kimkataba
uliopo kati ya mwanachama na chama chake. Hivyo, endapo mwanachama
anayechuliwa hatua za kiidhamu siyo kiongozi wa kitaifa wa chama cha
siasa, basi Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia mgogoro
huo wa uanachama., labda chama cha siasa na mwanachama husika kwa hiari
yao wamuombe Msajili wa Vyama vya Siasa kuwasuluhisha.
Isipokuwa,
endapo mwanachama husika ni kiongozi wa kitaifa wa chama, basi Msajili
wa Vyama vya Siasa anayo mamlaka ya kuingilia mgogoro huo ili
kujiridhisha kuwa, mwanachama husika amesimamishwa au kufukuzwa
uanachama wake kwa kuzingatia Katiba na Kanuni za chama husika, kwa
sababu kusimamishwa au kufukuzwa uanachama wake kunaathiri nafasi yake
ya uongozi wa kitaifa.
HITIMISHO
Hivyo,
kwa kuwa kifungu cha 10(f) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258
kinahitaji chama cha siasa kuwasilisha orodha ya viongozi wake wa
kitaifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, na kwa kuwa kifungu 8A(1)
kinampa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuhifadhi taarifa za viongozi
wa kitaifa wa Vyama vya Siasa na kwa kuwa pia Kanuni ya 5(1) ya Kanuni
za Usajili wa Vyama vya Siasa toleo namba 111 la mwaka 1992, inakitaka
kila chama cha siasa kuwasilisha taarifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa
panapotokea mabadiliko katika uongozi wa taifa.
Aidha,
Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mantiki ya majukumu yanayobebwa na
vifungu hivyo, anao wajibu wa kuhakikisha taarifa za mabadiliko ya
uongozi anazoletewa na chama cha siasa ni sahihi, kwa maana ya
kujiridhisha kuwa mabadiliko hayo ya uongozi, yamefanywa na mamlaka
halali ya chama na pia yametekelezwa kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za
chama husika. Hatua hiyo inafanyika, ili kuepuka kupokea na kuhifadhi
taarifa ya mabadiliko katika uongozi wa kitaifa wa chama cha siasa
ambayo siyo halali, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika.
Kwa
mantiki hiyo basi, nikijielekeza kwenye vifungu vya Sheria
nilivyoainisha hapo juu, ni dhahiri kwamba, Msajili wa Vyama vya Siasa
anayo mamlaka na wajibu wa kisheria, kuchunguza mabadiliko katika
uongozi wa kitaifa wa chama yaliyofanyika na masuala yote yanayohusu na
mabadiliko hayo. Mfano, pale ambapo mwanachama ni kiongozi wa kitaifa wa
chama cha siasa Msajili anapaswa kujiridhisha kuwa, mwanachama husika
amesimamishwa au kufukuzwa uanachama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni za
chama, kwa sababu kusimamishwa au kufukuzwa uanachama wake, kunaathiri
nafasi yake ya uongozi wa kitaifa.
EmoticonEmoticon