Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), leo saa 6:00
usiku litafunga tena dirisha la usajili baada ya kulifungua jana kwa saa
48 na imebainika kuwa timu tatu zaidi zilikuwa na dosari katika usajili
hivyo kufanya ongezeko la kutoka timu nane zilionekana kwa haraka
mapema wiki hii mara baada ya dirisha kufungwa Agosti 6, 2016.
Timu hizo kwa ujumla zilikuwa na dosari ya ama kutokusajili kabisa au
kutokamilisha usajili wa ushiriki wa ndani kwa msimu wa 2016/2-17. Timu
tatu nyingine zilizobainika leo Agosti 14, 2016 katika mtandao ni
pamoja na Toto African ya Mwanza na Stand United ya Ligi Kuu Tanzania
Bara kadhalika Arusha FC ya Arusha ambayo msimu huu itashiriki Ligi
Daraja la Pili (SDL).
Hadi tunatuma taarifa hii usajili ulikuwa ukiendelea kwa mfumo wa
mtandao (TMS) ikiwa na maana ya Transfer Matching System, lakini
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limerejea kanuni za usajili
hivyo kuzitoza faini timu zilizokuwa na dosari. Faini imetozwa kwa
viwango tofauti kulingana na mashindano.
Timu zinazohusika na usajili wa mtandao ni zile zinazoshiriki Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes
(SFDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) na adhabu ya kushuka daraja na
kwenda kushiriki Ligi ya Wilaya kisha Ligi ya Mabingwa Mikoa (RCL)
ambayo usajili wake ni wa kutumia karatasi.
Timu za Ligi Kuu ambazo zilikatiwa mawasiliano baada ya kushindwa
kuwahi tarehe ya mwisho ya usajili ni Young Africans ambayo haikusajili
kabisa. Kwa kufanya makosa hayo, kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya
Vodacom, Young Africans imeadhibiwa faini ya shilingi milioni tatu (Sh.
3,000,0000). Young Africans imetozwa faini hiyo kwa kutosajili jina hata
moja kabla ya Agosti 6, 2016.
Timu nyingine za Ligi Kuu ambazo hazikukamilisha usajili angalau
kufikisha wachezaji 18 ni African Lyon ya Dar es Salaam, Stand United ya
Shinyanga na Toto African ya Mwanza ambazo kila timu imetozwa faini ya
shilingi milioni moja (Sh.1,000,000).
Kwa timu za Daraja la Kwanza la StarTimes (SFDL), Coastal Union ya
Tanga pekee imetozwa faini ya shilingi milioni moja (Sh.1,000,000)
wakati timu nyingine za daraja hilo, Kiluvya United na Friends Rangers
za Dar es Salaam pamoja nna Panone, zimetoswa faini ya shilingi laki
tano (Sh. 500,000) kila moja.
Kadhalika kwa timu za Daraja la Pili (SDL), ambazo ni Kitayose ya
Kilimanjaro, Mashujaa ya Kigoma na Arusha FC ya Arusha, zimetozwa faini
ya shilingi laki tano (Sh. 300,000) kila moja. Faini hiyo ni kwa timu na
uongozi husika hauna budi kuilipa mara moja, kwani TFF haitatoa leseni
za wachezaji kama timu haijalipwa faini hiyo.
Kanuni zinazozungumzia usajili ni Sura ya 10 inayozungumzia usajili
na 11 inayozungumzia Adhabu Zihusuzo Usajili Na Uhamisho kadhalika
Uhamisho Nje ya Nchi.
EmoticonEmoticon