RAIS MWINYI:SERIKALI INAJIPANGA UJENZI WA MAGHALA YA CHAKULA

January 08, 2025

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa Ujenzi wa Maghala ya Kuhifadhia Chakula ili kuwa na Uhakika wa Chakula hivyo kujitokeza kwa Sekta binafsi kuanza kujenga ghala ni jambo linalopaswa kuungwa Mkono.


Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipofungua ghala la Kuhifadhia chakula Gando , Wilaya ya Wete ,Mkoa wa Kaskazini Pemba linalomilikiwa na Kampuni ya Yasser Provision .

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali inalenga Kuwapunguzia Mzigo wa Gharama Wafanyabiashara wanaoleta chakula nchini ili kuwepo kwa Unafuu wa bei kwa Wananchi.

Rais Dk.Mwinyi ameielezea njia nyengine ni kuwa na Ushuru Maalum kwa Bidhaa zinazopelekwa Pemba .

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Mpango wa kuifungua Pemba Kiuchumi una dhamira thabiti ya kuhakikisha Bei za bidhaa Muhimu zinashuka na kutoa unafuu wa maisha kwa Wananchi.

Amefahamisha kuwa Ujenzi wa Bandari za Mkoani,Shumba Mjini na Wete ambao utaanza karibuni ni miongoni mwa hatua muhimu ya Kuwawezesha Wafanyabishara kuleta Mizigo yao Moja kwa moja Pemba kutoka nchi wanazoagiza ili kupunguza gharama za mzunguko wa Usafirishaji.

Vilevile Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali inajipanga Kutafuta njia Bora za kupunguza gharama za chakula kwa Wananchi wa Pemba .

Ufunguzi wa ghala hilo ni miongoni mwa Shamrashamra za Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.





Share this

Related Posts

Previous
Next Post »