Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John (wa kwanza kushoto)
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko TBL Kushila Thomas pamoja na Meneja
Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria (wa kwanza kulia)
wakionyesha kinywaji cha Ndovu Red Malt mara baada ya kuzindua kinywaji
hicho jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e
Salaam ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi
wake. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John akiongea wakati wa
Uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika jana katika mgahawa wa
305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam ambapo wateja zaidi ya
50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake.
Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria amesema:
“Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake
ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na
zinazokwenda na wakati katika soko”.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Damian Soul akitoa burudani katika
uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika jana katika mgahawa wa 305
The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko TBL, Kushila Thomas (wa kwanza kushoto)
akijadiliana jambo na Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John
(katikati) pamoja na mgeni mwaliko aliyefika katika uzinduzi wa bia ya
Ndovu Red Malt uliofanyika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni
jijini Dar e Salaam.
Wageni waalikwa wakijipatia bia ya Ndovu Red Malt.
Wageni waaalikwa wakibadilisha nawazo huku wakijipatia kinywaji cha Ndovu Red Malt.
Wageni waliohudhuria uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam.
Kinywaji cha Ndovu Red Malt.
Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John(kushoto) akiwa na Msanii
wa Kuchora Picha Bwana Lute (katikati) wakionyesha furaha yao mara baada
ya uzinduzi wa bia hiyo.
Maua yaliyohudumia tukio hilo.
Katika
mkakati wake wa kuendelea kuwaletea wateja wake bidhaa zenye bora wa
hali ya juu, kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imezindua bia
mpya inayojulikana kama Ndovu Red Malt, bia ambayo imetengenezwa kwa
kimea kwa asilimia 100 na ikiwa ni mwendelezo wa ubunifu wenye ubora wa
bia ya Ndovu Special Malt inayoongoza kwa ubora na bia pendwa kwa
watumiaji wengi wa bia nchini.
Bia
ya Ndovu Red Malt imegundulika na kutengenezwa hapa nchini Tanzania ili
kukidhi ladha ya wanywaji wa bia ikiwa na ubora wa kiwango cha juu na
yenye ladha ya pekee kwa kulinganisha na aina nyinginezo za bia zilizopo
kwenye soko.
Uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt umefanyika katika mgahawa wa 305 The
Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam Julai 20 mwaka huu ambapo
wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake.
Mbali
na kuwa na ladha ya aina yake inayoleta burudani kwa watumiaji wake
kutokana na kutengenezwa kwa Shahiri kwa asilimia kubwa pia bia ya Ndovu
Red Malt inavutia kwa mwonekano wake wa rangi kuwa na rangi ya uwekundu
kwa mbali.
Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria amesema:
“Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake
ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na
zinazokwenda na wakati katika soko”.
Alisema
utengenezwaji wa bia ya Ndovu Red Malt kwa kutumia Shahiri kwa asilimia
asilimia100 kunaleta upekee wa bia hii kwa kulinganisha na bia zingine
kwenye soko na ina ladha tamu na mwonekano wake wa kuvutia ambao
unaiongezea thamani.
Kwa upande wake, Mpishi Mkuu wa Bia wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Cavin Nkya, alisema kuwa bia hii mpya ya Ndovu Red Malt
inazinduliwa ikiwa ni uthibitisho wa uwezo wa kampuni katika kuwapatia
watanzania kinywaji chenye kiwango cha kimataifa na chenye ubora wa hali
ya juu.
“Ndovu
Red Malt ni bia ya daraja la kwanza inayodhihirisha dhamira yetu ya
kuwapatia wateja kinywaji ambacho daima wametamani kukipata kikiwa
kimesheheni radha murua nay a kipekee,” alisema Nkya.
Nkya alimalizia kwa kusema kwamba matokeo mazuri katika utayarishaji
kinywaji hiki ni kutokana na uchanganyaji mahiri na wa umakini wa nafaka
bora zinazozalisha hapa nchini ambazo zinazotumika kutengeneza bia
Ndovu Red Malt.
Bia
hii ina kiasi cha kilevi cha asilimia asilimia 4 na inapatikana katika
chupa zenye muundo maridhawa zenye ujazo wa mililita 375 ,kama zilivyo
aina nyingi za bia zinazozalishwa na kampuni ya TBL zilizopo sokoni.
Sasa, bia ya Ndovu Red Malt itaanza kupatikana sehemu zote nchini ambako
kampuni inasambaza bidhaa zake kuanzia wiki hii kwa gharama ya shilingi
2,000/ kwa bei ya reja reja.
EmoticonEmoticon