VODACOM WAFANYA GULIO LA SIMU KIJITONYAMA, JIJINI DAR

June 12, 2016

Afisa wa Vodacom huduma kwa wateja, Jesca Mnosi, akitoa maelezo ya simu halisi na zisizo halisi kwa wananchi waliotembelea banda la Vodacom kwenye maonyesho ya simu yaliyoanza jana Juni 11, 2016 kwenye viwa nja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa simu wa Vodacom,Gabriel Mvamba, (kulia), akimpatia maelezo ya kitaalamu ya kutofautisha simu halisi na simu isiyo halisi, mteja wa kampuni hiyo alipotembelea banda la Vodacom kwenye maonyesho ya simu orijino kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Juni 1, 2016.

Afisa wa Vodacom kitengo cha huduma kwa wateja, Eunice Dominic, akimpatia maelezo mteja wa Vodacom alipotembelea banda la kampuni hiyo ya simu kwenye maonyesho ya simu orijino, Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam Juni 11, 2016
Wananchi wakipatiwa maelezo juu ya tofauti ya simu halisi (Original) na simu zisizo halisi (Fake), kutoka kwa maafisa wa kampuni ya simu ya Vodacom wakati wa maonyesho ya simu kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Juni 11, 2016. Maonyesho hayo yanakuja huku zikiwa zimebaki siku 5 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuzifungia simu zote zosizo halisi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »