Mkuu
wa mkoa wa mbeya ameagiza halmashauri zote mkoa wa Mbeya kukamilisha
utengenezaji wa madawati ifikapo JUNI 20 na sambamba na agizo hilo
ametaadharisha juu ya takwimu za Madawati Hewa kwa lengo la kuficha
ukweli
Kwa takwimu zilizopo Mkoa wa Mbeya
una upungufu wa madawati 32,000 na mpaka sasa utengenezaji wa madawati
umefikia asilimia 95 na ametoa hadi tarehe 20 juni kila halmashauri iwe
imekamilisha
Kuhusu udhibiti wa takwimu za
madawati hewa ameagiza kila Mkuu wa shule apokee madawati kwa maandishi
na yenye ubora kwa idadi Ile ile iliyobainishwa awali kuwa Ndiyo
upungufu wa madawati katika Shule zao
Amewataka
wanafunzi na walimu kuyatunza madawati wanayokabidhiwa ili kutoa nafasi
kwa serikali, wadau na wananchi kushughulikia changamoto zingine kama
ujenzi wa nyumba za walimu,madarasa na vyoo.