KIKAO CHA
TFF, YOUNG AFRICANS
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), leo Juni 7, 2016 limefanya
kikao cha pamoja na uongozi wa Klabu ya Young Africans.
Kikao hicho kilifanyika ofisi ya TFF iliyoko Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Ilala jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi
kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine; Kaimu Mkurugenzi wa
Sheria na Uanachama, Elliud Mvella; Makamu Mwenyekiti wa Young Africans,
Clement Sanga na Katibu Mkuu wa Young Africans, Baraka Deusdedit.
Baada ya mazungumzo, Rais wa TFF, Malinzi ametoa maelekezo yafuatayo:-
1.
Mchakato
wa Uchaguzi wa Young Africans uendelee.
2.
Mchakato
huo usimamiwe na Kamati ya Uchaguzi ya Young Africans chini ya uangalizi wa
Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
3.
Wale wote waliochukuliwa fomu za uchaguzi wa
Young Africans katika ofisi za TFF washirikishwe kwenye mchakato huo.
Mwisho, Rais wa TFF Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wanachama na wapenzi wa Young Africans na kuwa na umoja na
mshikamano kuelekea uchaguzi huo muhimu wa kwa mustakabali wa klabu.
TFF YATEUA KAMATI YA LESENI
ZA KLABU
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeteua Kamati ya
Leseni (Club Licensing Committee) ambayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi
ya leseni kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza na kutoa uamuzi kwa
kuzingatia Kanuni ya Leseni ya Klabu.
Wajumbe
walioteuliwa kwenye Kamati hiyo inayoundwa kwa mara ya kwanza ni Wakili Lloyd
Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), David
Kivembele, Hamisi Kissiwa na Prof. Mshindo Msolla.
Klabu
zinatakiwa kuchukua fomu za maombi TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa
kazi ambapo zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya Kanuni husika zitapatiwa
leseni husika ili zishiriki michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la
Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016/2017.
Kwa
klabu ambazo zitashindwa kukidhi matakwa ya leseni yanayolenga kuhakikisha
mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangaji matokeo katika
maeneo matano ya wachezaji (sporting), viwanja (infrastructure), utawala
(administrative and personnel), umiliki wa klabu (ownership) na fedha
(financial), hazitapa leseni hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki ligi.
Klabu
ambazo zitanyimwa leseni na kutoridhika na uamuzi huo, zitakuwa na fursa ya
kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF. Kwa mujibu wa Ibara ya
5(3) ya Kanuni ya Leseni ya Klabu ya TFF, Kamati hiyo ndiyo inayosikiliza
rufani zinazopinga uamuzi wa Kamati ya Leseni ya TFF.
Wajumbe wanaounda Kamati hiyo ni Wakili Alloyce Komba (Mwenyekit), Wakili
Abdallah Gonzi (Makamu Mwenyekiti), Dk Francis Michael, Abdallah Mkumbura na
Wakili Twaha Mtengela. Klabu zote zinahimizwa kuchukua fomu za maombi mapema
ili kutoa muda wa kutosha kwa TFF kupitia maombi yao na kufanya uamuzi kwa
wakati muafaka.
TFF YATOA KALENDA
YA MWAKA, USAJILI KUANZA JUNI 15
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), limetoa kalenda ya msimu mpya wa mashindano na matukio ambako
baada ya mapumziko ya wachazaji yanayoishia Juni 10, 2016.
Kalenda
inaonesha kipindi kinachofuata sasa ni usajili unaotarajiwa kuanza Juni 15,
2016. Usajili huo unaanza na uhamisho wa wachezaji ambako utaanza Juni 15, 2016
hadi Julai 30, 2016.
Kwa
mujibu wa Kalenda hiyo, timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa
2016/2017 zitaanza kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15, 2016 hadi
Juni 30, mwaka huu.
Kwa
upande wa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), watatumia kipindi cha
Juni 15, 2016 hadi Juni 30, 2016 kutangaza usitishwaji mkataba wa wacheaji. Usajili
wa utaanza Juni 15 hadi Agosti 6, kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara.
Pingamizi
itakuwa ni Agosti 7 hadi 14, 2016 kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya
kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, 2016 wakati usajili hatua ya pili
utaanza Agosti 17, 2016 hadi Septemba 7, 2016 na kitafuatiwa kipindi cha
kipindi cha pingamzi hatua ya pili kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14, 2016.
Septemba
15 hadi Septemba 17, 2016 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya
pili,
Ratiba
hiyo inasema kwamba timu zinatakiwa kuandaliwa
kuanzi Juni 15 2016 hadi Julai 15, 2016 ambako kuanzia Julai 16, 2016
hadi Agosti 14 ni kipindi cha mechi za kirafiki za ndani na nje. Ratiba ya Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka kati ya Julai 16 hadi Agosti 14.
TFF
YATANGAZA KOZI ZA UKOCHA
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) kupitia Idara ya Ufundi, imetangaza kozi nne (4) za Leseni
za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinazotarajiwa kuanza Juni 20, 2016 katika
mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam.
Kwa
Mkoa wa Mwanza, TFF itaendesha kozi ya leseni Daraja C. kozi hiyo inatarajiwa
kuanza Juni 20, 2016 hadi Julai 4, mwaka huu ambako baadhi ya washiriki 29
wamekwisha kujiandikisha ingawa bado kuna nafasi 11 ili kutimiza darasa la
wanafuzni 40.
Sifa
za watakaochukua kozi hiyo ni kuwa kuwa na cheti ngazi ya kati (intermediate)
na umahiri (activeness).
Hii
ni kozi ya CAF itakayoendeshwa na TFF na kwamba watu wenye ndoto za kuwa
makocha wa mpira wa miguu wanaruhusiwa kuomba.
Kwa
Jiji la Mwanza na mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, kozi hiyo inaratibiwa na
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF, Vedastus Rufano anayepatikana kwa
Namba ya simu 0753 772068 na Mwalimu atakuwa Wilfred Kidao ambaye ni Mkufunzi
wa ukocha anayetambuliwa na CAF.
Mchango
kwa ajili ya mkufunzi na uendeshaji Sh. 200,000 kwa kila mwanafunzi.
Kozi
nyingine ni ya leseni Daraja B ambayo itafanyika kuanzia Julai 1, hadi Julai
16, mwaka huu mkoani Morogoro. Kozi hiyo ambayo mchango wake ni Sh. 300,000 kwa
mwanafunzi tayari ina wanafunzi 35 na zimebaki nafasi tano tu na utaratibu wa
kuijiunga unaratibiwa na Ofisi ya Idara ya Ufundi ya TFF iliyoko Uwanja wa
Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kozi
nyingine ya leseni Daraja B inaratibiwa jijini Dar es Salaam ambayo kuanzia
Julai 1, hadi Julai 16, mwaka huu ambako washiriki wa kozi hiyo ni ya TFF
makocha ambao tayari walifanya kozi ya FIFA-IOC iliyofanyika Oktoba, 2014 hivyo
kwa sasa wanatakiwa kuthibitisha kushiriki kabla ya Juni 15, 2016 katika ofisi
ya Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.
Nafasi
pia zipo kwa washiriki wengine nje ya kundi la wale wa Oktoba, 2014 na kwamba
sifa ni kuwa na Leseni Daraja C na awe amewahi kufanya kazi ya ukocha angalau
kwa mwaka mmoja na zaidi. Mchango wa kozi hiyo ni Sh 300,000.
Kadhalika kozi nyingine ji ya Leseni Daraja A ambayo itafanyika kuanzia Julai 17, 2016
hadi Julai 31, mwaka huu kwa hatua ya kwanza yaani Module 1 wakati Module 2
itafanyika Novemba, mwaka huu. Mchango wa kozi hiyo la Leseni Daraja A ni Sh
600,000 ambayo inalipwa kwa pamoja.
Wakufunzi wa kozi hiyo ya juu ni Makocha Salum Madadi na Sunday Kayuni,
kabla ya CAF kumleta mtoa tathimini ya matokeo ya makocha hao kabla ya kutoa
leseni ya daraja husika.
Washiriki wa kozi hiyo wanatarajiwa kuwa makocha wa timu zinazoshiriki
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwani msimu wa mwisho wa makocha wa
Leseni Daraja B na C ni msimu wa 2016/2017.
Kuanzia msimu wa 2017/2018 hakuna kocha anayeruhusiwa kuongoza timu kwa
kukaa kwenye benchi la ufundi kama hana sifa ya Daraja B na C. Msimu huu wa
2016/2017 ni nafasi ya mwisho kwa makocha wenye leseni madaraja ya chini kukaa
au kuongoza timu za zinazoshiriki VPL.