Msanii
wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jioni
hii akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa
jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka
Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP
Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo
Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Msanii
huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kupiga ‘Live Music’
katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini,
Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama,
Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi
watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.
Msanii
wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akiondoka katika hoteli ya
Hyatt Regency-The Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza
kwenye Jembeka Festival 2016 ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu
za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la
Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF
Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM. Kulia ni Meneja wa
Hoteli hiyo, Timothy Mlay.
Meneja
Masoko wa CFAO Motors Group, Attu Mynah ambao wamedhamini usafiri
uliotumika kumwendesha msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo
gari aina Mercedes Benz GLE 350 D ya mwaka 2016 katika picha ya
kumbukumbu na Msanii huyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere.
Msanii
wa kimataifa Neyo aki-show love na walinzi maalum kabla ya kuelekea
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa
safari ya Mwanza.
Msanii
wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum
aina ya Mercedes Benz GLE 350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO
Motors Group.
Msanii
wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili uwanja wa
ndege wa Mwalimu JK Nyerere akiwa amezungukwa na walinzi maalum
alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
Msanii
wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili kwenye uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mlinzi wake
wakielekea jijini Mwanza leo jioni.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla
(t-shirt ya blue) na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo
wakijianda kupanda ndege ya Shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea jijini Mwanza. Shirika la
Ndege la Fastjet ni miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akiwa na ‘crew’
iliyoambatana na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo
wakipanda ndani ya ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa
wadhamini wa Jembeka Festival 2016 kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea
jijini Mwanza.
EmoticonEmoticon