Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza na madaktari wa wa
Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar na nchini Uingereza waliokuwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifanya matibabu ya moyo, haflaa hiyo
imefanyika jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Taasisi yake ndio kiungo
cha kuunanisha taasisi zilizoshiriki kuokoa maisha ya watoto wenye
matatizo ya moyo.
Naibu
waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Khamis Kigwangala akizungumza hatika hafla ya kufunga kambi ya
madakitari wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es
Salaam na kuwaaga madaktari wa nchi hizo.
Picha ya pamoja ya madaktari bingwa wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti za nchi tatu.
MADAKTARI
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamefunga kambi ya Madaktari wa tiba
ya Moyo wa kutoka Saudi Arabia, Uingereza na Qutar na baaadhi ya
madaktari wenye utaalam wa tiba ya matatizo ya moyo hapa nchini.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri
akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya
moyo kutoka nchi za Saudi Arabia, Uingereza na Qutar jijini Dar es
Salaam leo amesema kuwa kambi hiyo imejumuisha pamoja taasisi nne kutoka
nchi tatu tofauti.
Abri
amesema taasisi zilizoshiriki kambi ya Moyo Muhimbili ni Muntada Aid ya
Uingereza, Timu ya Madaktari kutoka Saudi Arabia, Taasisi ya Araf
kutoka Qutar na taasisi ya Dhi Nureyn ya hapa nchini na Taasisi ya
Jakaya Kikwete.
Amesema
kuwa kambi hii ya sasa imefanikiwa kuwatibu watoto wenye matatizo ya
moyo 66 ambao walikuwa wamepangwa kusafirishwa nje ya nchi kwaajili ya
matibabu sasa wametibiwa hapa nchini na kuokoa mabilioni ya fedha za
serikali.
Kwaupande wake Naibu
waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Khamis Kigwangala amewashukuru madaktari kutoka taasasisi hizo kwa
kuja hapa nchini na kuokoa watoto wenye matatizo ya moyo 200 ambao
wametibiwa hapahapa nchini.
Naibu
waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Khamis Kigwangala akizungumza hatika hafla ya kufunga kambi ya
madakitari wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es
Salaam na kuwaaga madaktari wa nchi hizo.
Katibu
mkuu na mkurugenzi wa Muntada Aid, Sheikh Khalid Sukeir akizungumza
katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo
jijini Dar es Salaam leo.
Kiongozi wa Madaktari, Jamil Al Ataa akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa Balozi wa Qatar, Wajih Al Uteibly akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akizungumza
katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka
taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akimkabidhi zawadi ya ngao Kiongozi wa Madaktari, Jamil Al Ataa wakati wa hafla
ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne
tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akikabidhiwa zawadi katika hafla
ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne
tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri.
Naibu
waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Khamis Kigwangala akikabidhiwa zawadi wakati wa hafla
ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne
tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Picha na Avila Kakingo.
Picha na Avila Kakingo.