Mratibu
wa Magonjwa ya Mlipuko Mkoa wa Dar es Salaam, Vicktoria Bulla (kulia),
akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa afya wakati akifungua
semina ya siku moja ya ugonjwa wa kipindupindu Dar es Salaam jana, kwa
niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa mgeni
rasmi. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Umma,
Hellen Semu na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Ufuatiliaji wa Magonjwa
ya Mlipuko wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Janeth Mghamba.
Semina hiyo iliandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la
Afya Duniani (WHO)
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Ofisa
Habari wa Wizara ya Afyaaaa na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura
(kulia), akibadilishana mawazo na mwenzake katika semina hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
Mada mbalimbali kuhusu ugonjwa huo na magonjwa ya mlipuko zikiendelea kutolewa.
Semina ikiendelea.
Wadau wa Afya wakiwa kwenye semina hiyo.
………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI
wa jiji la Dar es Salaam asilimia 70 kati yao wanatumia maji yasiyo
salama ambayo yanachangia kwa kiwango kikubwa kukithiri kwa magonjwa ya
mlipuko.
Hayo
yalibainishwa Dar es Salaam juzi na mtaalam wa afya kutoka idara ya
kinga kitengo cha afya na mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk.Theophil Likingaga katika semina ya waandishi wa habari ya
siku moja iliyoandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la
Afya Duniani (WHO) iliyohusu ugonjwa wa kipindupindu.
Dk.
Likingaga alisema asilimia hiyo kubwa ya watanzania kutumia maji yasiyo
salama imetokana na Shirika la Maji safi na Taka (DAWASCO), kuhudumia
asilimia 30 tu ya wananchi wa Dar es Salaam hivyo kuwa changamoto.
Alisema
pia asilimia 15 tu ya wananchu wa Dar es Salaam ndiyo waliounganishwa
kwenye mfumo wa maji taka hivyo kyfanta tatizo la uhaba wa maji safi na
utunzaji wa mazingira kuwa kubwa.
“Hayo
ndiyo baadhi ya maeneo ambayo tumeyaona pia suala la uuzaji matunda
kiholela, biashara za vyakula pia imekuwa ikichangia kuenea kwa ugonjwa
wa kipindupindu,” alisema Dk.Likangaga.
Alisema
wizara hiyo imejitahidi kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu kwa kugawa
dawa za kusafisha maji pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
Likangaga
alisema serikali kupitia DAWASCO imejitahidi kufunga vioski katika
maeneo mbalimbali na kusambaza maji kwa kutumia magari ili wananchi
wapate maji safi na salama.
Kwa
upande Mtaalam wa Maabara ya Taifa, Dk.Theophil Malibiche alisema tangu
ugonjwa wa kipindupindu uanze Agosti 15 mwaka huu, wamefanya vipimo
1071 ili kubaini vimelea vya kipindipindu.
Alisema kati ya hizo sampuli 668 sawa na asilimia 62 zimebainika kuwa na vimelea vya kipindupindu.
Kwa
upande wake, Ofisa Afya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Emmanuel Mwandepa
alisema serikali inaendelea kuangalia mbinu mbadala ya kutoa huduma ya
maji safi kwa wananchi.
Alisema
kutokana na mkakati huo wameanzisha kampeni yq nyumba kwa nyumba ambayo
itakuwa inakagua mazingira pamoja na ubora wa visima vya maji.
Aliongeza kutokana na mpango huo visima vifupi vya maji vitafungiwa ili kupunguza ugonjwa wa mlipuko.
EmoticonEmoticon