Makamu
wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto),
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tuzo ya
utoaji huduma bora waliyoipokea nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi
Oktoba kutoka kwa kampuni ya Business Initiative Directions (BID).
Pamoja naye kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes, Bw. Lanfang
Liao.
Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes, Bw. Lanfang Liao akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tuzo ya utoaji huduma
bora waliyoipokea nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi Oktoba kutoka kwa
kampuni ya Business Initiative Directions (BID).
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Mwandishi Wetu
Kampuni
ya Business Initiative Directions (BID) ya nchini Ufaransa imeitunuku
kampuni ya StarTimes kutoka nchini tanzania tuzo ya World Quality
Commitment (WQC) kwa utoaji huduma bora kwa wateja wake.
Sherehe za tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya 29 ziliyofanyika jijini Paris ambapo makampuni mbalimbali yalishinda yalishiriki.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuonyesha tuzo
hiyo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao
amesema kuwa hiyo ni habari njema si tu kwa kampuni bali kwa taifa kwa
ujumla kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.
“Tuzo
hii imetolewa jijini Paris, Ufaransa mwishoni mwa mwezi Oktoba ambapo
kampuni ya Business Initiative Directions (BID) ndio waandaaji wakuu wa
tuzo hizi ambazo zimefanyika mara ya 29 kwa mwaka huu.” Alisema Bw. Liao
“Utolewaji
wa tuzo huu ulihusisha marais, wakurugenzi, viongozi wa makampuni na
wafanyabiashara kwa ujumla ambao walikuwa wanapendekeza majina ya
kampuni inayostahili tuzo hiyo kutoka sehemu mbalimbali duniani.”
Katika
upigaji huo wa kura ambao hufanyika kwa siri bila ya hata kampuni
inayopigiwa kura kujua. Baada ya upigaji huo wa kura kampuni ya
StarTimes ambayo ndiyo pekee kutoka nchini Tanzania kujinyakulia tuzo
hiyo ya heshima.
“Kwa
niaba ya kampuni ya StarTimes ningependa kuchukua fursa hii kwanza
kabisa kuwatangazia wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa wao ndio
sababu kubwa mpaka sisi kutunukiwa tuzo hii. Pili, ningependa watanzania
wafahamu kuwa ushindi wa tuzo hii sio wa kampuni pekee bali ni kwa
Tanzania kwa ujumla kwani StarTimes ndio kampuni pekee iliyotunukiwa
tuzo hii.” Aliendelea bosi huyo
“Hivyo
basi, ningependa kuwashukuru wateja wetu lakini kikubwa zaidi ni
serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka
mazingira mazuri kwa kampuni zinazokuja kuwekeza nchini kuwahudumia
wananchi wake. Tunawashukuru wadau kama vile Tanzania Investment Center
(TIC), TCRA, na wizara zote bila ya kusahau vyombo vya habari ambavyo
tumekuwa navyo bega kwa bega katika shughuli zetu.” Aliongezea
“Ni kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji nchi na wananchi wake wananufaika na kusonga mbele kimaendeleo.”
“Kwa
kuhitimisha, ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru tena watanzania
kwa kuendelea kutuamini na kutuunga mkono katika shughuli zetu na wakae
mkao wa kula kwa kampeni zetu kabambe zinazoendelea kuzinduliwa hivi
karibuni.” Alihitimisha