Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi,
Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.
Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili
kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa
Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muung ano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es
Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK)
Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa
mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
EmoticonEmoticon