![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjQa3ruDqpOVemqwrAbAvyauR59fV9c7XfiaGIKJVKku9wqieF_lVFzBzNuSqvg055v-6TMoqPeh_-HVM5QJiQc65mz5Dkc_lJz1GddP22tJ1343V4zB0s0buTvZjQrZwGLFt9j2bWXP0g/s640/1.jpg)
Mmoja
wa wafanyakazi wa Chama Cha Albino, Christina Mbedi akielezea namna
Chama cha Albino kinavyofanya kazi zake kwa Meneja wa Chapa na
Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale wakati wa ziara ya viongozi wa
Zantel ofisini kwao. Anayetizama kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Umoja
wa Albino Tanzania, Ernest Kimaya.
Meneja
wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale akikabidhi msaada wa
vifaa vya mawasiliano kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Albino
Tanzabua, Ernest Kimaya. Wanaotazama nyuma ni baadhi ya viongozi wa
Chama cha Albino.

Tanzania, Ernest Kimaya. Anayetazama nyuma ni mmoja wa viongozi wa Chama
cha Albino.
Viongozi wa Chama cha Albino na Zantel wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Viongozi wa Zantel kutembelea ofisi zao.
- Yaiunganisha ofisi ya chama cha albino na huduma ya mtandao pamoja na mawasiliano ya simu
Dar es
Salaam, 8/10/2015: Uongozi wa Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo
umetembelea ofisi za Chama cha Maalbino Tanzania, ziara yenye lengo la
kujifunza zaidi kuhusu Chama cha Maalbino kinavyofanya kazi pamoja na
kuboresha ushirikiano baina yao.
Pamoja
na kuzungumza na viongozi wa chama cha Maalbino, uongozi wa Zantel pia
umekabidhi huduma za simu, kwa kuwapa namba maalumu pamoja na
kuwaunganisha na huduma ya mtandao.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Progress
Chissenga alisema huu ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya Zantel na
Chama Cha Maalbino.
‘Leo
tumeamua kuja kuwatembelea wenzetu wa Chama cha Maalbino ili kujionea
namna wanavyofanya kazi, na msaada huu wa intaneti pamoja na huduma ya
simu tuliyokabidhi leo itawawezesha viongozi na watendaji wa chama cha
albino kupiga simu bure kwa mwaka mzima, lakini pia itarahisisha
mawasiliano baina yao na viongozi wengine wa chama kutoka mikoani’
alisema Chissenga.
Katika
ziara hiyo, viongozi wa Zantel na Chama cha Maalbino Tanzania
walijadiliana maeneo mengine ya kuongeza ushirikiano baina yao katika
kuhakikisha chama cha Maalbino kinatekeleza majukumu yake zaidi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Bwana Ernest
Kimaya, alisema wanaishukuru kampuni ya Zantel kwa kuendelea kuwaunga
mkono katika juhudi zao za kuhakikisha mauaji ya albino yanamalizika
nchini.
‘Tunawashukuru
Zantel kwa kuendelea kutuunga mkono na msaada huu waliotukabidhi leo,
unaonyesha kuwa wana nia ya dhati ya kushirikiana na chama chetu’
alisema Kimaya.
Ziara hii ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel na Chama cha Maalbino Tanzania, ambao ulilenga kusambaza elimu juu ya ulemavu.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjQa3ruDqpOVemqwrAbAvyauR59fV9c7XfiaGIKJVKku9wqieF_lVFzBzNuSqvg055v-6TMoqPeh_-HVM5QJiQc65mz5Dkc_lJz1GddP22tJ1343V4zB0s0buTvZjQrZwGLFt9j2bWXP0g/s640/1.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjQa3ruDqpOVemqwrAbAvyauR59fV9c7XfiaGIKJVKku9wqieF_lVFzBzNuSqvg055v-6TMoqPeh_-HVM5QJiQc65mz5Dkc_lJz1GddP22tJ1343V4zB0s0buTvZjQrZwGLFt9j2bWXP0g/s640/1.jpg)
Mmoja
wa wafanyakazi wa Chama Cha Albino, Christina Mbedi akielezea namna
Chama cha Albino kinavyofanya kazi zake kwa Meneja wa Chapa na
Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale wakati wa ziara ya viongozi wa
Zantel ofisini kwao. Anayetizama kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Umoja
wa Albino Tanzania, Ernest Kimaya.
Meneja
wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale akikabidhi msaada wa
vifaa vya mawasiliano kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Albino
Tanzabua, Ernest Kimaya. Wanaotazama nyuma ni baadhi ya viongozi wa
Chama cha Albino.
Meneja
wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale akikabidhi msaada wa
vifaa vya mawasiliano kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Albino
Tanzania, Ernest Kimaya. Anayetazama nyuma ni mmoja wa viongozi wa Chama
cha Albino.
Viongozi wa Chama cha Albino na Zantel wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Viongozi wa Zantel kutembelea ofisi zao.
- Yaiunganisha ofisi ya chama cha albino na huduma ya mtandao pamoja na mawasiliano ya simu
Dar es
Salaam, 8/10/2015: Uongozi wa Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo
umetembelea ofisi za Chama cha Maalbino Tanzania, ziara yenye lengo la
kujifunza zaidi kuhusu Chama cha Maalbino kinavyofanya kazi pamoja na
kuboresha ushirikiano baina yao.
Pamoja
na kuzungumza na viongozi wa chama cha Maalbino, uongozi wa Zantel pia
umekabidhi huduma za simu, kwa kuwapa namba maalumu pamoja na
kuwaunganisha na huduma ya mtandao.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Progress
Chissenga alisema huu ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya Zantel na
Chama Cha Maalbino.
‘Leo
tumeamua kuja kuwatembelea wenzetu wa Chama cha Maalbino ili kujionea
namna wanavyofanya kazi, na msaada huu wa intaneti pamoja na huduma ya
simu tuliyokabidhi leo itawawezesha viongozi na watendaji wa chama cha
albino kupiga simu bure kwa mwaka mzima, lakini pia itarahisisha
mawasiliano baina yao na viongozi wengine wa chama kutoka mikoani’
alisema Chissenga.
Katika
ziara hiyo, viongozi wa Zantel na Chama cha Maalbino Tanzania
walijadiliana maeneo mengine ya kuongeza ushirikiano baina yao katika
kuhakikisha chama cha Maalbino kinatekeleza majukumu yake zaidi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Bwana Ernest
Kimaya, alisema wanaishukuru kampuni ya Zantel kwa kuendelea kuwaunga
mkono katika juhudi zao za kuhakikisha mauaji ya albino yanamalizika
nchini.
‘Tunawashukuru
Zantel kwa kuendelea kutuunga mkono na msaada huu waliotukabidhi leo,
unaonyesha kuwa wana nia ya dhati ya kushirikiana na chama chetu’
alisema Kimaya.
Ziara hii ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel na Chama cha Maalbino Tanzania, ambao ulilenga kusambaza elimu juu ya ulemavu.
EmoticonEmoticon