Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewateua wakuu wa wilaya wapya 13 na kuwahamisha vituo vya kazi wengine
saba.
Wakuu wa wilaya 13
walioteuliwa ni Shaaban Athuman Ntanambe ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Chato, Mkoa wa Kagera; Thabisa Mwalapwa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Hanang, Mkoa wa Manyara; Richard Kasesera ambaye anakuwa Mkuu wa
Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Ruth Msafiri ambaye anakuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma na Abdallah Njwayo ambaye anakuwa Mkuu
wa Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Wakuu wa Wilaya wengine
wapya ni Asumpta Mshama ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe,
Mkoa wa Njombe; Mohammed Mussa Utaly ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya
Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma; Dauda Yasin ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya
Makete, Mkoa wa Njombe; Honorata Chitanda ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Ngara, Mkoa wa Kagera; Vita Kawawa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kahama, Mkoa wa Shinyanga na Christopher Ng’ubyagai ambaye anakuwa Mkuu
wa Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida.
Wakuu wengine wapya ni
Hawa Ng’humbi ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mkoa wa
Shinyanga na Mrisho Gambo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mkoa
wa Kigoma.
Wakuu wa wilaya
waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye anatoka Mkalama,
Mkoa wa Singida kwenda Wilaya ya Arusha, Mkoa wa Arusha; Wilson E
Nkambaku ambaye anahamishiwa Arumeru, Mkoa wa Arusha kutoka Kishapu,
Mkoa wa Shinyanga; Francis Miti ambaye anahama Wilaya ya Hanang, Mkoa wa
Manyara kwenda Monduli, Mkoa wa Arusha na Jowika Kasunga ambaye
anahamia Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa kutoka Monduli .
Wengine waliohamishwa ni
Muhingo Rweyemamu kutoka Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe kwenda Wilaya
ya Morogoro; Hadija Nyembo ambaye anahamia Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa
Tabora kutoka Uvinza, Mkoa wa Kigoma na Benson Mpyesya ambaye anahamia
Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma kutoka Kahama.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.