MAMA TUNU PINDA ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA

July 08, 2015

????????????????????????????????????
Muonekano wa banda la PRIDE Tanzania liliyopo katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar-es-salaam maarufu kama Sabasaba.
PRIDE Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linalotoa huduma za kifedha zenye masharti nafuu kwa wafanya biashara ndogondogo na wakati ambalo lina lengo la kuondoa umasikini nchini.
????????????????????????????????????
Wananchi wakiingia ndani ya banda la PRIDE Tanzania kujionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wajasiriamali wanaowezeshwa na PRIDE Tanzania.
????????????????????????????????????
Mke wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda (kulia), akiwa ndani ya banda la PRIDE kujione bidhaa za wajasiriamali kutoka Mikoa mbalimbali wanaowezeshwa na PRIDE (kushoto), Meneja Mkuu wa PRIDE Tanzania, Shimimana Ntuyabaliwe wakifurahia jambo wakati wakijionea bidhaa hizo.
????????????????????????????????????
Mjasiriamali, Venture Manase (kulia), akimuonesha Mke wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda (kusho),moja ya gauni la wax alilolishona.
????????????????????????????????????
Mke wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda (kushoto) akiangalia gauni la batiki alipotembelea banda la kwetu Afrika liliopo ndani ya banda la PRIDE (katikati), mjasiriamali, Rajabu Kngalu, na kulia ni mjasiriamali Asha Sendege.
????????????????????????????????????
Mke wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda (kulia), akiangalia moja ya viungo vya chakula alipotembelea banda la PRIDE (kushoto), Meneja Mkuu wa PRIDE Tanzania, Shimimana Ntuyabaliwe.
????????????????????????????????????
Mke wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda, na Meneja Mkuu wa PRIDE Tanzania, Shimimana Ntuyabaliwe wakifurahia viungo vya chakula vinavyotengenezwa na mjasiriamali Mwanamke, Mariam Kimbu.
????????????????????????????????????
Meneja Mkuu wa PRIDE Tanzania, Shimimana Ntuyabaliwe akimkabidhi Mke wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda mfuko wenye machapisho na vijarida mbalimbali vya PRIDE Tanzania mara baada ya kumaliza kutembelea banda hilo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la PRIDE Tanzani wakipata maelezo namna ya kujiunga na vikundi vya mikopo kutoka kwa Afisa Mwezeshaji, Edward Ng’wandu.
????????????????????????????????????
 Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Bi Jacqueline Maleko (katikati), akipata maelezo ya virutubisho vinavyotengezwa kwa kutumia mbegu za matunda kutoka kwa mjasiriamali ,alipotembelea banda la PRIDE Tanzania kujionea bidhaa hizo (kushoto), Meneja wa Tawi la PRIDE Tanzania lililopo Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Elivictoria Bruno.
????????????????????????????????????
Picha ya Pamoja.
????????????????????????????????????
Wafanyakazi wa PRIDE Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja nje banda la PRIDE ambalo liko kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar-es-salaam maarufu kama Sabasaba.
Picha zote na Philemon Solomon-Fullshangweblog.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »