Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Elisha Mwampashi awataka vijana kujituma kuafanya kazi na kuacha kukaa vijiweni

May 26, 2015


 katibu  wa  UVCCM mkoa  wa  Iringa, Elisha Mwampashi wa  pili kulia akiwa na katibu  mkuu  wa UVCCM
Taifa Bw  Sixtus Mapunda.
………………………………………………..
 na fredy mgunda,iringa
Akizungumza na mtandao huu katibu wa uvccm mkoa wa iringa ELISHA MWAMPASHE alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.
“Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema  ELISHA MWAMPASHE
ELISHA MWAMPASHE ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.
“Vijana mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema  ELISHA MWAMPASHE
Lakini ELISHA MWAMPASHE amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
ELISHA MWAMPASHE  ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
Mbali na hayo ELISHA MWAMPASHE amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Ameendelea kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.
Aidha ELISHA MWAMPASHE amewataka vijana wa Manispaa ya Iringa, wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao ili waweze kujiajiri na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
“Tukiungana pamoja ni rahisi kufanikiwa kiuchumi, hakuna njia njia nyingine kwa sababu dhamana yetu vijana ni umoja tu, jiungeni kwenye vikundi vya ujasiriamali,”alisema ELISHA MWAMPASHE.

Alisema maeneo mengi ambayo vijana wameungana wameweza kukopeshwa, na wanaendesha shughuli zao za kiuchumi bila wasi wasi, jambo hilo linawezekana.
Alisema mpaka sasa wanayo zaidi ya Sh Milioni 10, ambazo wamekuwa wakikopeshana kwa riba naafuu.
Alifafanua kuwa mara nyingi vijana wa stendi wamekuwa wakiachwa nyuma kwenye shughuli za kimaendeleo jambo ambalo, limewafanya waungane.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »