USHINDI wa mabao 4-0 hii leo umetosha kabisa kuifanya Mgambo Shooting ya Tanga kunyakua pointi tatu zote muhimu kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Polisi Morogoro mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Mkwakwani.
Viashirio vya ushindi huo vilianza kuonekana mwanzo wa mtanange huo ambapo Mgambo Shooting waliingia uwanjani hapo wakiwa na hari mpya katika mechi hiyo iliyokuwa na patashika ya aina yake.
Bao la kwanza la Mgambo shooting limefungwa na Full Maganga dakika ya 31 baada ya kumalizia faulu iliyopigwa na Mohamed Samata baada ya mchezaji wa polisi Moro Labani Kambole kumfanyia madhambi Malimi Busungu.
Bao la Pili limefungwa na Malimi Busungu baada ya kumalizika krosi iliyopigwa na Fully Maganga dakika 38 na kutinga wavuni na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika mgambo 2-0,Polisi .
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo katika dakika ya 71 Mgambo waliongeza bao la tatu lililoweka kimiyani na Malimi Busungu huku Salim Azizi Gilla akiipatia Mgambo bao la nne na kuhitimisha karamu hiyo ya mabao
EmoticonEmoticon