MAVETERAN KUCHUKUA KESHO KATIKA BONANZA VIWANJA VYA POPATLALY TANGA.

April 05, 2015
Katibu Mkuu wa Timu ya Tanga Middle Age Veteran,Nuru Jumbe akiwaonyesha waandishi wa habari jana kombe ambalo litashindaniwa katika bonanza la Maveteran litakalofanyika Jumatatu likishirikisha timu saba,kushoto ni Katibu Msaidizi wa timu hiyo,Ramadhani Sadiki na kulia ni Nahodha wa timu hiyo Thomas Semdoe

Katibu Mkuu wa Timu ya Tanga Middle Age Veteran,Nuru Jumbe akiwaonyesha waandishi wa habari jana medali ambazo watapewa washindi katika bonanza la Maveteran litakalofanyika Jumatatu likishirikisha timu saba,kushoto ni Katibu Msaidizi wa timu hiyo,Ramadhani Sadiki na kulia ni Nahodha wa timu hiyo Thomas Semdoe


JUMLA ya timu saba kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini zinatarajiwa kushiriki katika bonanza la Maveteran ambalo linatarajiwa kufanyika kesho(Leo) Jumatatu ya Aprili 6 mwaka huu kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly mjini hapa.
Akizungumza jana, Katibu wa Klabu ya Tanga Middle Age Veteran,Nuru Jumbe alisema ambao ndio waandaaji wa bonanza hilo alisema kuwa litashirikisha michezo mbalimbali.

Katibu huyo alizitaja timu hizo kuwa ni Zanzibar Veteran,Morogoro
Veteran,Mandingo Veteran,Disuza SC,Mango Garden Veteran ya  Dar es Salaam,Tanga Middle Age Veteran na Kitambi Noma ya Dar es Salaam.

Aliitaja michezo ambayo itafanyika siku hiyo kuwa ni Mpira wa Miguu, Kurusha Tufe, Kuvuta Kamba na Kukimbiza Kuku ambapo bingwa atazawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo Medali na kombe.

Aliongeza kuwa malengo kuu ya bonanza hilo ni kukuza vipaji vya soka sehemu ya kazi na kuendeleza undugu na kutangaza biasha pamoja na kuweka mahusiano mazuri na wafanyakazi wengine.

Aidha alisema wanamshukuru mdau wa michezo mkoani hapa,Yanga Omari kwa hatua yake nzuri ya kulidhamini bonanza hilo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza mkoani hapa.

  “Tunamshukuru sana mdau huyu kwa kuona umuhimu wa jambo hilo na kulifadhili lakini tunapenda kuwataka wadau wengine wajitokeze kulifadhili bonanza hili “Alisema Katibu huyo.

Bonanza hilo litaanza saa mbili asubuhi ambapo pia kutakuwa na mchezo wa kushindania kucheza mziki ambapo washindi wote watakabidhiwa zawadi na mgeni rasmi, Khalid Abdallah ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »