BILIONEA DANGOTE AKAGUA UFUKWE ATAKAOJENGA BANDARI YAKE YA KISASA MTWARA

April 23, 2015

 Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Alhaji Dangote akipata maelezo kuhusu eneo alilopewa na Serikali ya Kijiji cha Mgao lenye ukubwa wa heka 2500 sawa na hekta 1000. Anatarajia kuanza kujenga bbandari hiyo mapema mwaka huu.
 Ndege iliyomleta Dangote ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara tayari kwenda kukagua eneo atakapojenga bandari yake.
 Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti
 Dangote akilakiwa na Esther Baruti
 Alhaji Dangote akilakiwa na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Majanbu
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisalimiana na Alhaji Dangote

 Alhaji Dangote akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (kushoto) Mwakilishi wake hapa nchini, Esther Baruti na Balozi Dk, Majanbu
 Alhaji Dangote akizungumza na Esther Batuti
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dedengu akimtambulisha Alhaji Dangote kwa wananchi alipowasili katika Kijiji cha Mgao, ambapo amepewa Dangote  eneo la ujenzi wa Bandari
 Alhaji Dangote akisaini katika kitabu cha wageni alipowasili katika Kijiji cha Mgfao kukagua eneo la ujenzi wa Bandari pamoja na kiwanja alichopewa na wanakijiji kujenga makazi yake.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Abdulrahman Shaa
 Wananchi wakiangalia msafatra wa Alhaji Dangote uliokuwa unakwenda eneo asmbapo bandari itajengwa.
 Alhaji Dangote akiwa na viongozi wa Kijiji cha Mgao pamoja na wananchi akikagua uwanja heka mbili na nusu aliyopewa kwa ajili ya kujenga makazi yake katika kijiji hicho
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa  na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo.
 Msafara wa Alhaji Dangote ukielekea eneo patakapojengwa Bandari
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa akihojiwa na wananchi kuhusu maufaa watakayopata wanakijiji endapo Nadari hiyo ikijengwa
 Alhaji Dangote akizungumza na wanahabari kuhusu ujenzi wa bandari hiyo
 Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa
 Alhaji akijadiliana jambo na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha saruji, Kushoto ni Paschasia Ngaiza Mama Mzazi wa Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais wa Tanzania, Premy Kibanga ambaye pia alikuwepo kwenye ziara hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akimuaga Alhaji Dangote uwanjani hapo
 Alhaji Dangote akiteta jambo na mwakilishi wake hapa nchini, Esther muda mfupi kabla ya kupanda ndege kwenda Ethiopia na hatimaye Lagos, Nigeria.
 Alhaji Dangote akiaga
 Dedengu akijadiliana jambo na Esther
 Balozi wa Nigeria nchini, akizungumza jambo na Dendengu pamoja na Esther. Kulia ni Paschasia Ngaiza
Ndege iliyombeba Alhaji Dangote na ujumbe wake ikiondoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara
Tagged:

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »