Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) pichani leo jioni imefanya mazoezi
ya mwisho tayari kwa kuwakabili Wenyeji wao Tanzania Timu ya (Taifa
Stars) mchezo utakaochezwa kesho jumapili saa 10.30 jioni katika Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wakibadilishana Mawazo wakati Wachezaji wa Malawi wanajifua mara ya mwisho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jioni ya leo.
Tiketi
za mchezo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo vya Uwanja wa
Nyamagana na uwanja wa CCM Kirumba kwa bei za sh. 5,000 kwa mzunguko,
sh. 12,000 kwa jukwaa kuu na sh.20,000 kwa viti vya jukwaa kuu maalum.
Taifa Stars inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa viwango vya FIFA
vilivyotolewa mwezi Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika wakiwa
nafasi ya 91 kwenye vinago hivyo.
Mayanga
amesema vijana wake wote 22 waliopo kambini wapo fiti, wamefanya
mazoezi kwa siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,
wachezaji wapo kwenye ari na morali ya juu, kikubwa wanachosubiri ni
kesho tu kushuka dimbani kusaka ushindi.
Aidha Mayanga amewaomba wapenzi wa mpira wa miguu waliopo jijini Mwanza
na mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa, kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani
kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo.
Tayari waamuzi na kamishina wa mchezo wameshawasili jijini Mwanza,
mwamuzi wa kati atakua ni Munyazinza Gervais kutoka nchini Rwanda,
akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda),
mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda), mwamuzi wa akiba
Martin Saanya kutoka Morogoro huku na Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza
kutoka Mwanza.
Baadhi ya Viongozi wa Soka wakiteta jambo Uwanjani hapo CCM Kirumba
EmoticonEmoticon