Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe, Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr, Balozi wa
Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu, Mwakilishi wa Chama cha Albino
Tanzania (TAS), Abdillah Omar sambamaba na wadau wengine wakishiriki
kuimba wimbo ‘Tanzania Tanzania’ kabla ya kuanza kwa shughuli nzima ya
hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye
viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.
Picha zote Othman Michuzi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akisoma hotuba yake.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar
Kweigyr akicheza muziki wa sambamba na Mwanamuziki wa Reggae,Jhiko
Manyika “Jhikoman” wakati wa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita
mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders
Club, jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers
Network ambao ni wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim Mushi.
- Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini
(Imetosha), Ally Masoud “Kipanya” akimkaribisha Balozi wa Harakati ya
Imetosha, Henry Mdimu ili kuzungumza na Watanzania waliofika kwenye
Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
EmoticonEmoticon