Jeshi la Magereza nchini
limemfukuza kazi askari wake wa Gereza Bariadi, Mkoani Shinyanga
(pichani) kwa kosa la kupatikana na fadha za bandia kinyume na Sheria za
Nchi.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi
iliyotolewa jana Machi 28, 2015 na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini, John Casmir Minja, askari Na. B. 6499 Wdr. Edmund
Masaga amefukuzwa kazi kwa fedheha kuanzia Machi 28, 2015 kwa kosa la
kulidhalilisha Jeshi mbele ya Umma kinyume na Kanuni 22(xlix) ya Kanuni
za Utumishi wa Jeshi la Magereza za Mwaka 1997.
Aidha, Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini, John Casmir Minja amekemea vikali vitendo hivyo kwani
ni kinyume cha Maadili na Utendaji ndani ya Jeshi la Magereza huku
akiwataka askari wote wa Jeshi la Magereza nchini kutenda kazi zao kwa
uadilifu na uaminifu mkubwa.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
Machi 29, 2015.
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
Machi 29, 2015.
EmoticonEmoticon