YANGA YAFUZU RAUNDI YA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO LICHA YA KUFUNGWA JANA

February 28, 2015




Yanga imefanikiwa kuingia raundi ya kwanza ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa BDF 11 ya Botswana kwa mabao 3-2.

Yanga imefuzu kwa bao la ugenini baada ya kufungwa jana mabao 2-1 na mchezo wa awali kushinda mabao 2-0 nyumbani Dar es Salaam

Kwenye mchezo huo hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Mrisho Khalfan Ngassa dakika ya 30 kwa kichwa, akimalizia pasi ya Amissi Tambwe ambaye alipokea krosi ya Simon Msuva.
Dakika ya 21, BDF walipata pigo baada ya beki wake, Othusitse Mpharitlhe kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kumfuatia kumchezea rafu winga wa Yanga, Simon Msuva.

Kipidi cha pili BDF walianza vizuri na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 49 kupitia kwa Mosimanyana aliyemalizia kazi nzuri ya Lerole.

Dakika ya 72 mshambuliaji Danny Mrwanda alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu beki wa BDF.

BDF walipata bao la pili dakika ya 85 kupitia kwa Kumbulani Madziba aliyewatoka mabeki wa Yanga kabla ya kumtungua Ally Mustafa ‘Barthez.’

Yanga SC watacheza na mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na Platinum ya Zimababwe katika Raundi ya Kwanza.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Barthez, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Cannavaro, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Danny Mrwanda na Mrisho Ngassa/Kpah Sherman dk87.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »