KAMATI
KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 28/8/2015,
kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na moja alasiri, kimeazimia
yafuatayo;Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, msanii wa Chama na Kada wa
muda mrefu Mheshimiwa John Damian Komba.
Mwenyekiti
wa CCM, Mhe Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kuwa msiba huo ni pigo
kubwa kwa Chama hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi na
pengo ambalo ni vigumu kuliziba.
CCM
imepata pigo na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti inatoa pole kwa familia,
ndugu, jamaa na marafiki wa Kapteni John Damian Komba.
Kazi yake kubwa ndani ya Chama itaandikwa katika historia iliyotukuka ya Chama Cha Mapinduzi.
>
Pia, kutokana na Kikao cha Kamati Kuu iliyopita iliyoiagiza kamati ya
maadili kuwaita na kuwahoji wanachama na viongozi watatu waliotajwa
kuhusika na kashfa ya Escrow.
@ Mheshimiwa Anna Kajumulo Tibaijuka
@ Mheshimiwa William Mganga Ngeleja
@ Mheshimiwa Andrew Chenge
Baada
ya Kamati ya Maadili kuwahoji, Kamati Kuu imeazimia kuwasimamisha
kuhudhuria vikao ambavyo wao ni wajumbe ikiwemo Kamati kuu kwa Mama
Tibaijuka na Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Mheshimiwa Chenge na
Ngeleja.,wakati ambapo kamati ndogo ya maadili ikiendelea na uchunguzi
wa kuhusika kwao katika kashfa hiyo.
>
Pia, Kamati Kuu imejadili suala la Adhabu iliyotolewa kwa wanachama
sita ambao walibainika kuvunja Kanuni na sheria za Chama kwa kuanza
Kampeni kabla ya wakati na imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuendelea
kuchunguza mienendo ya wanachama hao katika kipindi walichokuwa
wanatumikia adhabu zao. Na kisha taarifa hiyo ya Kamati ndogo ya maadili
itawasilishwa kwa Kamati Kuu.
EmoticonEmoticon