Meneja Mauzo wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugaano Kasambala, akimpa pole Ester Jonas, mama wa Yohana Bahati, mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino, aliuawa mkoani Mwanza, hivi karibuni. Mama huyo anatibiwa katika Hospitali ya Bugando baada ya kupata mareraha katika tukio la kuvamiwa na kuporwa mtoto wake. Kulia kwa Kasambala ni Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir mwenye miwani waliyeambatana katika safari hiyo kwa ajili ya kuwapa pole na kuwafariji.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MBUNGE wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir kwa ushirikiano na Taasisi ya Kifedha, inayojihusisha na mikopo ya Bayport Financial Services yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, Tanzania, walifanya ziara ya siku mbili jijini Mwanza kwa ajili ya kutembelea familia mbili zilizopoteza watoto wao wawili ambao ni walemavu wa ngozi.
Familia hizo ni ya Ester Jonas, mama wa marehemu Yohana Bahati na ile ya Sofia Juma mama wa mtoto Pendo Emmanuel, wote wakiwa ni watu wenye ulemavu wa ngozi, huku familia zote mbili zikipewa Sh Milioni 2 kila moja.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir mwenye miwani akimfariji mama wa Yohana Bahati (Ester Jonas) aliyelazwa Hospitali ya Bugando, Mwanza, pamoja na kumpaa mafuta ya kupaka kwa ajili ya watoto wake wawili ambao nao ni albino,. Kushoto kwa Mh Shaimar ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala na wafanyakazi wengine wa Bayport waliombatana pamoja kwenye msafara huo wa kutoa pole.
Akizungumza katika safari hiyo, Mbunge Shaimar alisema
ameendelea kusikitishwa na mauaji hayo ya albino yanayotoa haki ya kuishi ya
watu wote wenye ulemavu wa ngozi, huku akiitaka jamii kuacha kufavya vitendo hivyo visivyokuwa vya kiungwana kutokana na kudhulumu haki za kuishi za binadamu wenzao.
“Naumia juu ya vitendo hivi kwasababu na mimi nipo kwenye
kundi hili lawatu wenye ulemavu wa ngozi wanaoendelea kupukutika siku hadi
siku, hivyo tupambane na majangili haya, maana najua Mheshimiwa Rais, Dr Jakaya
Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wamekuwa wakiguswaa mno na matukio haya
yanayoichafua nchi yetu,' alisema Shaimar, ambapo pia aliishukuru Bayport Financial Services kuingia katika harakati za kupambana na mauaji ya albino nchini Tanzania.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyri (katikati), akizungumza
na binti aliyekutwa nyumbani kwa Ester Jonas, mama wa albino Pendo Bahati
aliyeporwa na haijulikani alipokuwa. Kulia kwake ni Meneja Mauzo wa Bayport
Financial Services, Lugano Kasambala, aliyeambatana na mbunge huyo.
Naye Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, alisema taasisi yao imeguswa na mauaji hayo na kuitaka jamii kushirikiana na viongozi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama katika kupambana vikali na watu wanaoendeleza kufanya unyama wa kuteka watu wenye ulemavu wa ngozi kwa sababu wanazojua wenyewe.
Alisema hali hiyo waliamua kufanya safari moja na mbunge Shaimar ambaye kiuhalisia ni balozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi, huku akiamini kwa ushirikiano huo unaweza kupunguza au kuondosha kabisa vitendo hivyo vya mauaji ya albino yanayoendelea kushika kasi katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara.
Wengine waliombatana kwenye ziara hiyo ni pamoja na Afisa
Ustawi wa Jamii Mwanza, Leah Linti, Katibu Tawala Msaidizi Crecencia Joseph,
Mweka Hazina wa Chama cha Albino Taifa (TAS), Abdullah Omari, Jeshi la Polisi
wilayani Misungwi, huku safari zote zikiwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Mkoa
wa Mwanzaa, Magesa Mulongo.
EmoticonEmoticon