UCHAWI WAMKIMBIZA ZARI BONGO

February 28, 2015

Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, akiwa na mpenzi wake  Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’
ISHU ya uchawi kwa wanawake wajawazito ndilo suala kubwa linaloingia kwenye hisia za baadhi ya watu hasa mimba inapokuwa changa, hofu hiyo sasa imemwingia mwandani wa Mbongo-Fleva anayeuza zaidi kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,  Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ ambaye anadaiwa kuikimbia Bongo kwa muda ili mimba yake isije kuchoropoka kama ilivyokuwa kwa akina Wema Sepetu na Penniel Mungilwa ‘Penny’
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa familia ya Diamond, hivi karibuni Zari aliondoka Bongo mara tu baada ya kurejea kutoka Zanzibar walikokuwa wameenda kula bata katika Msimu wa Valentine.
Chanzo hicho kilidai kwamba, wakati staa huyo mwenye maskani yake Afrika Kusini na Uganda akiwa Bongo maneno mengi yalisemwa na wengine kudiriki kuwapigia simu watu wa familia hiyo wakimtaka Zari aache tabia ya kujionesha na ujauzito wake kwani hawajui Wabongo vizuri.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »