Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akimueleza jambo Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Francis
Michael wakati wa mkutano na wasanii uliofanyika katika ukumbi wa uwanja
mpya wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni
na Michezo Prof. Herman Mwansoko akiongea na wasanii nchini na kuwaeleza
kuhusu umuhimu wa sekta hiyo kushiriki kikamilifu katika masuala ya kitaifa
hasa katika kipindi hiki cha kuelekea upatikanaji wa Katiba Mpya, Kulia ni
Katibu wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akiongea na wasanii nchini na kuwaasa wasanii kuielimisha na kuhamasisha
Jamii kuhusu Katiba Inayopendekezwa kupitia kazi mbalimbali za sanaa, wakati
wa mkutano na wasanii nchini uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Francis Michael akiongea na
wasanii nchini na kuwaeleza namna gani makundi mbalimbali yalivyoainishwa
kwenye Katiba Inayopendekezwa ikiwemo haki za wasanii tofauti na Katiba ya
Mwaka 1977.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akiongea na baadhi ya wasanii mara baada ya kuisha kwa mkutano huo leo Jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na
Michezo Dkt. Fenella Mukangara wakati wa mkutano huo.
EmoticonEmoticon