Kocha
Mkuu Coastal Union,James Nandwa kulia akilakiwa na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha mara baada ya kuwasilia mkoani
Tanga jana.
HAPA NI KOCHA NANGWA WA KWANZA KULIA AKIELEKEZWA JAMBO NA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA KUSHOTO NI KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI |
Kocha Mkuu Coastal Union,James Nandwa kulia akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha mara baada ya kuwasilia mkoani Tanga jana. |
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
ALIYEWAHI kuwa Kocha wa Kiungo
Mkenya, Victor Wanyama anayechezea soka lake kwenye klabu ya ,Southampton
nchini Uingereza James Nandwa ameingia mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu
ya Coastal Union ya Tanga.
Kocha huyo anachukua mikoba iliyoachwa na Kocha
Yusuph Chippo aliyekwenda nchini kwao Kenya kutokana na matatizo ya kifamilia
kuwa kwenye hali ambayo sio mzuri jambo ambalo lilipelekea kushindwa
kurejea nchini kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Akizungumza mara baada ya kutua jijini Tanga leo
ikiwemo kulakiwa na viongozi wa klabu hivyo wakiongozwa na Meneja wake ,Akida
Machai wakiwemo Katibu Mkuu pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji,Kocha huyo
alisema kuwa dhamira yake kubwa ni kuhakikisha anaipa mafanikio timu hiyo.
Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal
Union,Oscar Assenga amesema kuwa ujio wa kocha huyo utawezesha timu hiyo
kufikia malengo yao ambayo wamejiwekea ya kuhakikisha wanachukua ubingwa wa
Ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Assenga amesema kuwa kutokana na uzoefu aliokuwa
nao kocha huyo utawezesha kupelekea chachu kwa wachezaji waliopo kwenye kikosi
hicho kupambana wakiwa na lengo la kuipa mafanikio timu hiyo.
Kwa upande wake,Kocha Nandwa
amesema kuwa kitu cha kwanza ni kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake
iliyojiwekea ya kuwa timu bora Tanzania ili iweze kupata nafasi ya kushiriki
kwenye michuano ya kombe la shirikisho.
“Kwanza nashukuru
kupata nafasi ya kuifundisha Coastal Union nitahakikisha nitaifikisha timu hii
kwenye malengo waliojiwekea ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara
kutokana na uzoefu wangu niliokuwa nao “Amesema Nandwa.
Kocha Nandwa aliwahi kuzifundisha
timu za soka za Harambee Stars,AFC Leopard ya Kenya pamoja na Utalii ya Kenya
na kuipa mafanikio makubwa ikiwemo Ubingwa wa Ligi kuu nchini humo.
EmoticonEmoticon