HATIMAYE MISS TANZANIA 2014 SITTI ABBAS MTEMVU AMEJIVUA TAJI RASMI

November 08, 2014

Barua ya aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu aliyowaandikia Lino International Agency kuhusu uamuzi wake wa kujivua taji hilo.

HATIMAYE kampuni ya Lino International Agency imemvua taji aliyekuwa mrembo wa Tanzania 2014 (Redd’s Miss Tanzania 2014) Sitti Abbas Mtemvu kwa kosa la kudanganya umri katika mashindano hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga amesema kampuni yake imeamua kumvua  taji hilo mrembo huyo ambaye ni mtoto wa mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu.
Taarifa zinadai kuwa mrembo huyo aliitumia barua kamati ya uandaaji wa Miss Tanzania iliyoeleza uamuzi wake wa kuvua taji hilo.
Baada ya kukabidhiwa taji la Redd’s Miss Tanzania 2014 Oktoba 11, siku chache baadae Sitti alikumbwa na kashfa ya kudanganya umri baada ya kuonekana kuna utofauti wa umri kati ya leseni na pasipoti yake. Taji hilo litakabidhiwa kwa mshindi wa pili Lilian Kamazima.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »