Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia wananchi wa kijiji cha Matemanga wakati wa hafla ya uzinduzi
nyumba 480 za watumishi wa umma zilizojengwa na Taaasisi ya Benjamin
W.Mkapa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya(picha na Freddy Maro).
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Benjamin w.Mkapa Dkt Ellen Mkondya Senkoro(kushoto) akimuonesha Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete michoro na ramani za nyumba za watumishi wa
afya zilizojengwa na taasisi hiyo wkati hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo
uliofanyika katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru leo.Watatu
kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na wane kushoto
ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akikata utepe kuzindua mradi wa nyumba za watumishi wa afya zilizojengwa
na Taasisi ya Mkapa Foundation katika hafla iiyofanyika katika kijiji
cha Matemanga wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma leo.Jumla ya nyumba 480
zinajengwa katika halmashauri 48 nchini na miongoni mwa nyumba hizo 40
zipo katika mkoa wa Ruvuma.Taasisi ya Benjamin Mkapa iliingia mkataba na
Wizara ya Afya kutekeleza mradi wa miaka mitano(2011-2016) wa
uimarishaji wa mifumo ya Huduma za afya chini ya ufadhili wa mfuko wa
Dunia wa kupambana na ukimwi,kifua kikuu na Malaria(Global Fund).Wengine
katika picha kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin W.Mkapa Dkt.Ellen Senkoro, Mbunge
wa Jimbo la Tunduru Mhandisi Ramo Makani, Meneja wa Portfolio, Mfuko wa
Dunia wa Kupambana na ukimwi,kifua kikuu na Malaria Bi. Tatajana
Peterson, Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof.Anna Tibaijuka, Naibu
Waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri, Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa
jamii Kebwe Stephen Kebwe, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana
Saidi Mwambungu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kiwete
akiteta jambo na mkazi wa kijiji cha Ligela wilayani Namtumbo Bwana
Edwin Ngonyani wakati alipokuwa anahitimisha ziara yake wilayani
humo.Bwana Ngonyani ambaye alipata ulemavu baada ya kupoteza miguu yote
miwili katika ajali ya moto alimweleza Rais kuwa anapata taabu ya
kutafuta riziki kwakuwa anatambaa kwa taabu.Rais Kikwete alitoa ahadi ya
kumsaidia mlemavu huyo ili aweze kujikimu kimaisha.
EmoticonEmoticon