Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa
habari silaha aina ya SMG iliyokamatwa ikiwa na risasi mbili pamoja na
watuhumiwa watano ambapo mmoja kati ya watuhumiwa hao aliyefahamika kwa
jina moja la Rajab anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-36 alifariki
dunia baada ya kushambuliwa na wananchi huko katika kijiji cha Tura
wilayani Uyui. Aidha majambazi hayo yalikamatwa baada ya kufanya tukio
la unyang'anyi wa kutumia silaha ambapo yalifanikiwa kupora zaidi ya
shilingi milioni mbili na laki tatu na ndipo makachero wa Jeshi la
Polisi kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi walifanikiwa
kuyakamata yakiwa na silaha hiyo ambayo imedaiwa ilitumika katika tukio
la uporaji pamoja na Pikipiki mbili aina ya Sanlg |