Na Oscar Assenga, Lushoto.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga,Abdi
Makange amewataka vijana wilayani Lushoto kujituma na kufikiria namna ya kubuni
ajira mbadala ikiwemo kujikita katika masuala ya ujasiriamali ili kuweza
kuendesha maisha yao
badala ya kuendelea kutegemea ajira za kuajiriwa.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza na wajumbe wa kamati
ya utekelezaji ya umoja huo wilaya ya Lushoto(UVCCM)wakati wa ziara yake ya
kwanza ya kukagua na kuangalia uhai wa umoja huo pamoja na kufanya mikutano ya
hadhara inayofanyika mkoa mzima wa Tanga.
Makange alisema katika dhama hizi za utandawazi vijana
wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kubuni miradi mbalimbali ikiwemo kufanya
biashara na kufungua makampuni ambayo yataweza kutimiza ndoto zao katika
maisha.
“Vijana wengi
huathiriwa na ajira hasa wale wa vyuoni nataka kuwaeleza kuwa lazima mjitambue
sasa kwa kuelekeza nguvu zenu katika ajira za kujiari wenyewe kwa kuanzisha
makampuni ambayo yatawawezesha kusukuma
gurudumu la maendeleo yenu “Alisema Makange.
Aidha aliwaataka vijana kuangalia changamoto waliokuwa nazo
ili kuweza kukabiliana nazo na kuzipatia ufumbuzi lengo likiwa kuhakikisha
umoja huo unaimarika na kuwataka vijana walipo vyuoni kujitahidi kuingiza
wanachama wapya katika maeneo yao.
Mwenyekiti huyo aliwataka vijana hao kuwa mstari wa mbele
kukitetea chama hicho na kujenga mshikamano na kuachana na makundi yasiyokuwa
na tija lengo likiwa ni kuimarisha umoja huo mkoani hapa.
EmoticonEmoticon