MNDOLWA:NITATOA MILIONI 5 KWA VIJANA WATAKAOANDAA EKARI TANO ZA ALIZETI

December 21, 2013
Raisa  Said,Korogwe
MJUMBE wa  Halmashauri kuu  CCM  Taifa {NEC} Kupitia  Jimbo  la  Korogwe  vijijini  Dr. Edmund  Mndolwa  ameahidi  kutoa  mil. 5  kwa vijana ambao  wataandaa ekari  tano  za  shamba  la kulimia alizeti  lengo  likiwa kuwakwamua  kiuchumi.

Akizungumza   katika  mikutano  mbalimbali wakati  wa ziara  yake  ya  siku  za saba   jimboni humo  alisema  ameahidi  kutoa  pesa  hiyo  kwa  vijana  wakata  20  ambao  wataandaa   maeneo  ya  kulimia  alizeti.

Dk  Mndolwa  ambae  pia  ni mwenyekiti  wa  Wazazi  Mkoa wa  Tanga  alisema  kuwa  mpango  huo  utaweza kuwasaidia  vijana  wengi  kujiajili  na  kuepuka  kufanya  vitendo  viovu  na  kuacha  kukaa vijiweni  bila  ajira.

Mjumbe  huyo  wa  Halmashauri Kuu aliwaeleza  juu ya  kuona  umuhimu  wa  kuanzisha  zao  hilo ni kutokana   na kuona  kwa  muda  mrefu  watu  wamekuwa  wakikosa  chakula  na kipato  kutokana  nakutovuna  kwa  wingi  mazao  kama  mahindi  na  mihogo  ambayo  walikuwa  wakilima.

Hata  hivyo  alisema  kuwa  zao  la  alizeti  kwasasa ndilo  zao  la uchumi katika wilaya  ya  korogwe  ambapo  aliwataka  wakazi  wa  maeneo  hayo  kulithamini  na kulitunza  ili  liweze  kuwakomboa  kiuchumi   na  kuwapatia  kipato  kikubwa.

Mndolwa  alieleza  kama  vijana  wataandaa  mashamba  hayo  ataweza kuwasaidia  katika kila  kata  kuwapatia  250,000 za kuanzia  ili  wafanye  shamba  darasa  na  hatimaye  zao  hilo  kushamili katika jamii nzima.

  “ jamani  vijana  andaeni  maaeneo  ya  mashamba  ya  ekali tano  ili  tuweze  kuanza  kulima  alizeti  kama  mfano  wa  zao  hilo  ambalo  hapo awali  lilikuwa  halilimwi  hapa korogwe” Alisema  Dk  Mndolwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »