Na Oscar Assenga,Tanga
UMOJA wa waganga na wakunga wa
jadi Tanzania (UWAWATA) umeunda kamati ya wajumbe 10 watakaoshughulika tatizo la uharibifu ikiwemo kukomesha
mauaji kama vile ya Maalbino na vikongwe nchini.
Aidha Umoja huo uliwaagiza waganga na wakunga wa
tiba asilia nchini kujisajili kwenye umoja huo na kuacha kufanya shughuli
zao kibiashara na kwamba kazi ya tiba ni huduma na siyo biashara.
Akitangaza msimamo huo, kwenye mkutano mkuu wa Mkoa
uliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Sahare way jijini hapa,
Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja huo, Dk Rashid Tengeza alisema
kuwa Uwawata inajukumu la kuhakikisha matendo ya kikatili na
kishirikina yanakoma na kuifanya jamii na taifa kuwa na amani.
Kwamujibu wa Dk Tengeza ambaye pia aliongozana
na Katibu Mkuu wa taifa wa Umoja huo, Dk Daud Nyaki ni
kwamba chanzo cha mitafaruku,uchochezi na mauaji ni ramli
chonganishi zinazopigwa na waganga wa tiba asilia
wasiyowaaminifu.
“Sisi waganga wa tiba asili ndiyo wenye jukumu la
kulipoza taifa hili na kuwa la amani kwani majanga yanayotokea ni waganga wa
tiba asilia wasiyowaaminifu kujihusisha na matendo kama vile
uchochezi,mitafaruku na mauaji” alisisitiza Dk Tengeza.
Alisema ufike wakati waganga kudhibitiana wenyewe kwa
wenyewe na kwamba serikali inatarajia kuona matunda ya Umoja huo ikiwa ni
kukomesha mauaji ya vikongwe na albino ambayo hufanywa ama kuchochewa na
wachawi ama waganga matapeli.
Aidha alisema chini ya Umoja huo waganga ni wawe
kiungo kati ya serikali na wananchi ambao ni wateja wao na kufichua kila uovu
unaofanyika kwenye maeneo yao na kubainisha kuwa kila mganga atakaefanya
hivyo Umoja huo utakuwa mtetezi wake anapopata matatizo anapotoa tiba kwa wananchi.
Katika mkutano huo uongozi wa UWAWATA Mkoa
ulijaza nafasi za wajumbe zilizokuwa wazi ndani ya kamati ya
utendaji ambapo mbali na Mwenyekiti wa Mkoa, Allan Nkong’ota, makamu
mwenyekiti Bakari Mwinjuma. Katibu wa Mkoa ni Omari Sinde na Zaina
Mkama msaidizi wake.
Hata hivyo katika uchaguzi huo uliyosimamiwa na Dk Nyaki
iliundwa pia kamati maalumu ya Mkoa yenye watu kumi na kupewa
jukumu la kufichua uharifu, kukomesha waganga matapeli, rambaramba,wapiga ramli
chonganishi, mauaji ya albino na vikongwe.
Waliyochaguliwa kwenye kamati hiyo ambayo ilishirikisha
wataalamu kutoka taasisi mbalimbali nje ya Umoja huo, ni mwenyekiti wa
kamati, Juma Lukuwa, (mganga) katibu ni Dege Masoli ambaye ni mwandishi wa habari mkoani hapa
Aidha wajumbe ni Abdalla Hamissi,Swalehe Shamsham,Mayasa
Jabu,Mwajuma Bakari,Teresia Basilio,Mavumba Zuberi,Kulthumu Hussein akiwemo na
mwandishi wa habari Elizabeth Kilindi.
Mwisho
EmoticonEmoticon