MECHI YA YANGA, MTIBWA YAINGIZA MIL 97/-

October 07, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyochezwa jana (Oktoba 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Yanga na Mtibwa Sugar imeingiza sh. 97,557,000.

Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 46 lililochezeshwa na Isihaka Shirikisho kutoka Tanga walikuwa 17,313. Yanga ilishinda mabao 2-0.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,453,748.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,881,576.27.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,925,635.06, gharama ya kuchapa tiketi ni sh. 3,171,190 wakati gharama za mchezo ni sh. 7,155,381.04.

Kamati ya Ligi sh. 7,155,381.04, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,577,690.52 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,782,648.18.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »