NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MICHUANO ya Kombe la Mkonge Cup inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi kesho (leo) kwenye mashamba ya mkonge yaliyopo sehemu mbalimbali
hapa nchini.
Akizungumza na Tanga Raha, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano
hayo,Lai Mpuma alisema mashindano hayo msimu huu yanatarajiwa kuwa na ushindani
mkubwa kutokana na maandalizi yaliyofanywa na timu shiriki.
Mpuma alisema timu shiriki katika michuano hiyo
zimepangwa katika makundi manne ambapo katika kundi A kutakuwa na timu za China
State ambao watafugua pazia la mashindano hiyo kwa kucheza na New Msowero
katika uwanja wa soka Rudewa.
Alisema katika kundi B timu ya Toronto na Magoma
hizo ndio zitafungua pazia la michuano hiyo katika uwanja wa Toronto wakati Mkumbara
na Mazinde wao watacheza pia katika uwanja wa soka Mkumbara.
Aidha aliongeza kuwa katika kundi C timu
zitakazofungua pazia la mashindano hayo ni Kauzeni na Amboni Sp Mill katika
uwanja wa soka Kauzeni wakati Lugongo na Muheza Estate nao wakicheza kwenye
dimba la Lugongo.
Mwenyekiti huyo alisema michezo mengine itakayochezwa
siku hiyo ni Sakura ambao watacheza na Tancord kwenye dimba la soka Sakura huku
Mwera na Kumburu wakihitimisha mechi hizo katika uwanja wa soka Mwera.
EmoticonEmoticon