Na Oscar Assenga, Muheza.
KOCHA Mkuu wa timu ya Halmashauri FC ya Muheza, Benard
Mwalala (wa kwanza kulia katika picha juu) amesema ushindi walioupata dhidi yao na Lushoto Shooting ya wilayani
humo katika mchezo wa Ligi ya Mkoa wa Tanga ni ishara nzuri kwao kuendelea
kufanya vizuri mechi zao zifuatazo.
Mwalala alitoa kauli hiyo jana mara baada ya
kumalizika mchezo huo ambapo timu hiyo iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-0
mchezo uliochezwa uwanja wa soka Jitegemee wilayani hapa.
Katika mchezo bao la kwanza la Halmashauri
lilipatikana katika dakika ya 15 kupitia Ramadhani Msumi ambaye alipachika
mabao mawili na dakika ya 44.
Mpaka timu zote zinakwenda mapumziko, Halmashauri FC
walikuwa wakiongoza katika mchezo huo ambapo ulikuwa na upinzani kwa timu zote
kushambuliana kwa zamu.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote
ziliingia uwanjani hapo zikiwa na hari ya mchezo baada ya kufanya mabadiliko
kwa baadhi ya wachezaji wao.
Wakionekana kujipanga na kuwakamia wapinzani
wao,Halmashauri FC iliweza kuendeleza wimbi la ushindi langoni mwa Lushoto
Shooting na kufanikiwa kuandika bao lao la tatu kwenye dakika ya Gao Jaffari
dakika ya 75.
Mwalala alisema malengo yao msimu huu ni kuhakikisha
timu hiyo inafanya vizuri katika mashindano hayo ili iweze kupata nafasi ya
kushiriki Ligi ya Mabingwa wa mikoa na hatimaye ligi daraja la kwanza pamoja na
ligi kuu siku zijazo.
EmoticonEmoticon