WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Samia Suluhu amesema uandikaji wa katiba mpya unalenga kuijenga Tanzania ya sasa na siku zijazo hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwa makini katika kila hatua ili kuweza kufanikisha mchakato huo.
Suluhu alitoa kauli hiyo wakati akifungua Kongamano la
Wazanzibar waishio bara katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa na kusema kwenye mchakato huo,tume ya
mabadiliko imefanya kazi nzuri ya kusikiliza maoni ya wananchi kwenye maeneo na
makundi mbalimbali.
Alisema ofisi yake imeona umuhimu wa kufanya tathimini ya
miaka hamsini ya utekelezaji kwenye masuala ya muungano na kuweka mwelekeo
mzuri wa kushughulikia masuala hayo ikiwemo maoni yaliyokusanywa na tume ya
mabadiliko ya katiba.
“Kuna haja ya kupata
maoni ya makundi haya kwa umahususi wao,katiba ni mali ya Taifa na dira yetu
sote pamoja na mwongozo muhimu kwa taifa ili kuhakikisha linasonga mbele
“Alisema Waziri Suluhu.
Aidha alisema kwa kuzingatia misingi hiyo ni wajibu wa kila
mmoja wetu kubaini kuwa hakuna aliye na haki zaidi ya mwengine katika mchakato
huo na kueleza katiba bora ni ile inayotokana na watu pia inayoakisi matakwa ya
watu kwa kulenga kujenga na kustawisha maisha ya wana chi husika.
Aliongeza kuwa wakati huu mchakato wa katiba mpya unaendelea
ni vema kila mmoja wetu atambue kuwa nchi yetu ina bahati kubwa sana kwa mwenyezi
mungu kuijalia mchakato huo kuwa katika
mazingira mazuri ya amani na utulivu kwani ni nchi chache sana duniani
zilizojaliwa kuandika katiba zao katika mazingira hayo.
Alieleza kuwa nchi nyingi sana zinapofikia uamuzi wa kuwa na
katiba mpya baada ya machafuko, vita, mifarakano na hata mapinduzi
yanayosababisha umwagaji wa damu lakini watanzania wameamua kufanya jambo hilo
kwa dhamira njema na katiba inayokidhi mazingira ya sasa na
kuharakisha maendeleo kwa wananchi wake.
“Rai yangu kwa
mkusanyiko huu na watanzania wote kwa ujumla ni kwamba tuzidi kuvumiliana na kuwa watulivu katika mchakato huu na kila
mmoja wetu aweke mbele maslahi ya taifa
na katiba tunayoiandaa sasa iwe msingi mkuu wa kudumisha
amani,mshikamano na umoja wa taifa letu kwa kizazi cha sasa na kijacho “Alisema
Suluhu.
Mwisho.
EmoticonEmoticon