Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambayo
ni Tanga, Arusha , Kilimanjaro na Manyara wakizungumza na Waandishi wa Habari
juu ya fursa za uwekezaji katika kanda hiyo.
|
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa
akisisitiza jambo katika Mkutano huo.
|
Picha ya pamoja ya Wakuu wa Mikoa ya Kanda
yaKaskazini na baadhi ya viongozi wa TIC. Kutoka kushoto ni Mhe. Elaston John
Mbwilo, mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe.
Magesa .S. Mulongo , Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Leonidas E. Gama, Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mhe. Chiku Gallawa Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Kutoka
kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Bw. Abby Kagomba. Kwa
Habari zaidi kuhusu Mkoa wa Tanga tembelea tovuti yetu www.tanga.go.tz na Blog www.mkoatanga.blogspot.com. Stori
na Monica Laurent, Afisa Habari Mkoa wa Tanga.
|
NA MONICA LAURENT,PRO TANGA.
Kongano la Uwekezaji Kanda ya Kaskazini linatarajiwa kufanyika Septemba 26 na 27 mwaka huu katika Hoteli ya Mkonge Jiji la Tanga. Lengo kuu likiwa ni kukuza Uchumi na Kuongeza ajira Kanda ya Kaskazini.
Umuhimu wa Kongano hili ndio ulilosukuma Wakuu wa Mikoa wa Kanda ya Kaskazini kukutana leo katika Ukumbi wa kituo cha Uwekezaji ( TIC) na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali ili kuweza kuwatangazia Wananchi na Umma kwa ujumla kuhusu fursa za maendeleo zilizopo katika mikoa hii.
Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Mwenyeji wa Kongano hili Mhe. Chiku Gallawa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga amesema maandalizi ya Kongano hili yako katika hatua za mwisho.
Gallawa alisema mkoa wa Tanga uko tayari kupokea wageni/ wawekezaji"Tunategemea kupokea wageni/wawekezaji zaidi ya 600 kutoka ndani na nje ya Tanzania na ni imani yetu kwamba kupitia kongano hili hali ya Uchumi katika Kanda hii utaimarika”
Nao Wakuu wa Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga ambayo inaunda Kanda ya Kazkazini wamepata nafasi ya kunadi fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mikoa hiyo.Fursa nyingi zinapatikana kwenye Kilimo, Utalii, Viwanda, Ufugaji na Madini.
Ni wito kwa kila mwekezaji kutumia fursa hii kuwekeza katika mikoa hii ambayo imejaliwa kuwa na rutuba nzuri, hali ya hewa nzuri, madini mbalimbali, mbuga za wanyama n.k.
Kushiriki kwenye Kongano hili jiandikishe kwa fomu maalumu ambayo ipo kwenye tovuti ya Kanda www.investnorthernzone.go.tz kisha tembelea fursa za uwekezaji kwa kuchagua Mkoa husika.
EmoticonEmoticon