Baadhi
ya wadau na mashabiki wa soka Kisiwani Pemba wamevitaka vilabu vya ligi
kuu Visiwani Zanzibar , kuweka wasemaji wa Vilabu vya ili iwe ni rahisi
kwa mashabiki wa Vilabu hivyo kuweza kupata taarifa za timu zao .
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi Kisiwani Humo , wamesema kwa kukosekana kwa
wasemaji kunawanyima uhuru wa kuweza kupata taarifa juu wa vilabu vyao
,jambo ambalo linawafanya washindwe kufahamu usajili wa timu zao kabla
ya kuanza kwa ligi hiyo .
Khamis
Mohammed Kombo amesema kuwa ni tofauti na timu ya Tanzania Bara ambazo
zinawasemaji wao , ambapo mashabiki na wapenzi wa vilabu hivyo hupata
taarifa za usajili pamoja na maandalizi ya timu zao .
Hata
hivyo uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba
kikwazo cha kutokuwa na wasemaji wa timu ni katiba ambazo zinaruhusu
kuwa na makatibu wenenzi badala ya wasemaji wenye taaluma ya habari kama
ilivyo kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzani Bara .
Aidha
pamoja na katiba kutoruhusu kuwa na wasemaji wenye taaluma ya habari ,
lakini hata hizo nafsi za uwenezi ni bora wakapewa wanahabari ambazo
wanamapenzi na vilabu hivyo , ili waweze kuitumia taaluma yao kuwapasha
mashabiki juu kile kinachoendelea katika vilabu vyao.
Mmoja
wa Viongozi wa moja ya klabu inayoshiriki ligi Kuu Zanzibar (jina
tunalo)
alisema kuwa utaratibu wa kuwa na wasemaji ni mzuri , na kushauri
kufanyika kwa marekebisho katika katiba za vilabu ili kuwepo na wasemaji
ambao ni wanahabari .
Alisema
kuwa hata wandishi wa habari wanapohitaji kujua maandalizi pamoja na
usajili katika vilabu hivyo hushindwa kutambua ni kiongozi gani
anayeweza kutoa taarifa hizo , jambo ambalo linawafanya mashabiki na
wapenzi wa vilabu hivyo kusubiri ligi ianze ili wajue usajili wa
wachezaji .
EmoticonEmoticon