MOROCCO AICHIMBA MKWARA OLJORO JKT.

August 11, 2013


Na Oscar Assenga, Tanga.
KOCHA Mkuu wa timu ya Coastal Union ,Hemed Morroco amesema watahakikisha wanajipanga vyema ili kuweza kuchukua pointi tatu muhimu kwenye mechi yao ya ufunguzi wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi yao na JKT Oljoro itakayochezwa Agosti 24 katika uwanja wa Sheirh Amri Abeid mkoani Arusha.

Morroco alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na blog hii ambapo alisema mechi za majaribio walizocheza zimempa mwanga mzuri wa kujua kikosi chake kinahitaji kitu gani kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu.

Alisema kutokana na usajili mzuri ambao ulifanywa na timu hiyo matumaini yake ni kuchukua ubingwa wa ligi hiyo ili kuweza kucheza kombe la shirikisho kwani hayo ni malengo yake ya kucheza kombe hilo siku zijazo.

Morroco alisema wanatarajia kuondoka mkoani hapa siku moja kabla ya mechi yao na Oljoro JKT na kueleza watakachokwenda kukifanya mkoani Arusha ni kufuata pointi tatu muhimu.

Wakati huo huo,Timu ya 3 Pillars ya Nigeria na Coastal Union ya Tanga jana zilishindwa kutambiana baada ya kulazimishana sare ya kutokufungana katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ambapo kila timu ilikuwa ikilishambulia lango la mwenzie kwa zamu ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilitoka nguvu sawa licha ya Coastal Union kuonekana kukosa mabao ya wazi kutokana na wachezaji wake kukosa umakini.

Wakizungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo baadhi ya wadau wa soka mkoani hapa waliojitokeza walisifu kiwango kilichoonyeshwa na timu ya Coastal Union ambacho kilicheza vema licha ya kushindwa kufunga mabao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »